“Mapenzi ni kitu kingine kabisa, sikuwahi kujua ni kwa nini baadhi ya watu hufikia hatua ya kukatisha maisha yao kisa mapenzi, hakika mapenzi ni sumu kali sana maishani usipojiongoza,” alisema Johari
Saturday, 7 December 2013
"NIMEGUNDUA MAPENZI NI SUMU KALI MAISHANI USIPOJIONGOZA....." JOHARI
SIKU chache baada ya kuingia katika mgogoro na msanii mwenzake,
Chuchu Hans kwa madai ya kugombea penzi la Vincent Kigosi ‘Ray’,
muigizaji Blandina Chagula ‘Johari’ amesema amegundua mapenzi yanaumiza
na ni sumu mbaya maishani.
Blandina Chagula ‘Johari’.
Akizungumza na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita katika moja
ya mahojiano maalumu, Johari alisema mapenzi si kitu cha kuendekeza
kwani ni hatari na ndiyo maana baadhi ya watu hufikia hatua ya kuchukua
uamuzi mgumu wa kujiua.
“Mapenzi ni kitu kingine kabisa, sikuwahi kujua ni kwa nini baadhi ya watu hufikia hatua ya kukatisha maisha yao kisa mapenzi, hakika mapenzi ni sumu kali sana maishani usipojiongoza,” alisema Johari
“Mapenzi ni kitu kingine kabisa, sikuwahi kujua ni kwa nini baadhi ya watu hufikia hatua ya kukatisha maisha yao kisa mapenzi, hakika mapenzi ni sumu kali sana maishani usipojiongoza,” alisema Johari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment