Wilfried Zaha amechukua
hatua ya aina yake kukanusha taarifa zilizozagaa kwamba ana uhusiano wa
kimapenzi na mtoto wa kike wa kocha mkuu wa Manchester United David
Moyes.
Winga huyo mwenye miaka 21 alinunuliwa na Sir Alex
Ferguson kwa £15milllion lakini ameshindwa kupata nafasi ya kucheza
ndani ya kikosi cha kwanza chini ya David Moyes.
Kumekuwepo na
taarifa kwamba amekuwa hapewi nafasi ya kucheza na Moyes kwasababu ya
mahusiano yake na binti wa kocha huyo aitwaye Lauren.
Lakini Zaha -
ameonekana kukerwa sana na tetesi hizo - ametumia ukurasa wake wa
Twittet kuwaambia mashabiki 490,000 kwamba taarifa hizo sio za kweli.
'Sijawahi
kuwa na mahusiano ya kimapenzi wala kukutana na binti wa David Moyes,
hivyo jambo hilo haliwezi kuwa sababu ya kukosa kwangu nafasi katika
kikosi cha kwanza ...,' aliandika Zaha.
'Ningependa hizi taarifa
za uongo ziachwe kusambazwa….Nitaichezea Manchester United pindi kocha
atakapoana nipo tayari kufanya hivyo...'
Zaha aliichezea United
katika mchezo wa kombe la hisani lakini tangu wakati huo ameichezea
mechi moja tu ya mashindano dhidi ya Norwich City katika League Cup.
No comments:
Post a Comment