Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi
ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar,
Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Sepetu imetolewa hukumu yake
baada ya Wema kuomba iharakishwe kwakuwa alikuwa anasafari.
Kwa mujibu wa mtandao wa Global
Publishers, Wema sepetu amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu gerezani
ama faini ya shilingi laki moja kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa
baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo mawili ya kupiga na
kutukana.
Baada ya kusomewa hukumu hiyo wema
alitoa laki moja hiyo iliyokuwa ikihitajiwa na mahakama kabla ya
kuachiwa huru kuendelea na mishe zake nyingine
No comments:
Post a Comment