Hii ni aibu kwa taifa! ‘Makachero’ wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM)
iliyo chini ya Global Publishers wameibua uozo mwingine jijini Mwanza
baada ya kubamba tukio la kusikitisha na kufedhehesha la mtoto mwenye
umri wa miaka 12 akijiuza.
Uchunguzi
wa OFM jijini hapa wiki iliyopita umebaini kuwa vitendo hivyo
vinaonekana vya kawaida na kuzoeleka miongoni mwa wakazi wake, jambo
linalotia dosari kwa mji huo unaosifika kwa usafi wa hali ya juu wa
mazingira.
OFM ilishuhudia wimbi kubwa la watoto wa kike walio chini ya umri wa
miaka 18 wakijihusisha na biashara haramu ya kuuza miili nyakati za
usiku.
Awali taarifa za uwepo wa watoto hao jijini Mwanza zilipokelewa
katika ofisi za Global Publishers jijini Dar kutoka kwa baadhi ya
wasafiri na wakazi wa jiji hilo wakiomba kupelekwa kwa OFM kutokana na
suala hilo kutofanyiwa ufumbuzi na taasisi husika.
“Jamani hii ni aibu kwa taifa letu! Hapa Mwanza mjini kuna vibinti
vidogo sana vinauza miili, tunaomba OFM isibakie Dar pekee, njooni na
huku hali inatisha,” aliomba mkazi mmoja wa Mwanza.
OFM
huwa haipuuzi taarifa kutoka kwa vyanzo vyake hivyo iling’oa nanga
katika jiji la maraha na karaha la Dar na kutinga rasmi Jiji la Miamba
(Rocky City) Mwanza kufanyia kazi kilichosemwa.
Kweli watoa taarifa walikuwa na hoja kwani katika viunga vya Mwanza
Mjini maeneo ya Kauma jirani na Mnara wa Samaki kwenye Barabara ya
Nyerere, OFM iliwashuhudia watoto hao wakijiuza bila wasiwasi huku
wakilindwa na watoto wenzao wa jinsia ya kiume waliokuwa na chupa na
viwembe kama silaha zao.
Katika utafiti wake, mmoja wa ‘makamanda’ wa OFM alijifanya mteja kwa watoto hao ambapo alifanikiwa kuongea nao.
Kuhusu bei, mmoja alieleza kuwa huwa wanatoza shilingi 20,000 kwa kulala usiku mzima na elfu 5,000 kwa short time.
Maskini! Mtoto Aisha (12) alikuwa yupo tayari kuchukuliwa kwa
makubaliano yoyote ambapo alisema kinachomfanya kujihusisha na biashara
hiyo ni hali ngumu ya maisha na wazazi wake kushindwa kumsomesha.
Katika kazi hiyo ya OFM jijini Mwanza, mtoto huyo alidai kuwa
alipopelekwa shule ya msingi huko wilayani Sengerema, wazazi wake
walishindwa kumudu michango ya kila kukicha hivyo akabaki nyumbani hadi
alipotorokea jijini.
Akizungumza na OFM juu ya sakati hilo la kushamiri kwa biashara hiyo
haramu, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alisema: “Sina taarifa
yoyote kuhusiana na watoto hao wanaojiuza ndiyo nasikia labda nipate
muda wa kuzungumza na uongozi wa chini nitalichukulia hatua mara moja.”
No comments:
Post a Comment