Wednesday, 11 December 2013

Wanamgambo waanza kuondoka Tripoli

Wapiganaji wa jeshi la mgambo huko Libya wanaolaumiwa kwa ghasia mbaya mjini Tripoli tangu kuanguka kwa Moammar Ghadafi walianza kuondoka katika mji mkuu Jumatatu huku vikosi vya jeshi la Libya vikiingia kuhakikisha usalama mitaani.

Wanamgambo kutoka pwani ya mji wa Misrata walianza kuondoka kuelekea mashariki baada ya  kutokea ufyatuaji risasi kwa waandamanaji Ijumaa na kuchochea siku mbili za mapambano ambayo yaliuwa watu wasiopungua 46 na kuwajeruhi mamia wengine.

Pia Jumatatu naibu mkuu wa upelelezi nchini Libya, Mustafa Nuh aliachiwa huru na watekaji nyara wake siku moja baada ya kumkamata wakati akiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli.

Haikufahamika ni nani alimteka Nuh ambaye familia yake inatokea Misrata.

No comments: