Rais Zuma ametangaza siku 5 za maombolezo kitaifa na bendera
zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku
ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya
maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria
umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu
Bill Clinton na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya
viongozi ambao wamethibitisha kushiriki.
Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.
Mwili wake utawekwa katika jengo la serikali liitwalo Union Buildings
kuanzia Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya
kupelekwa kijijini Qunu kwa mazishi.
Hata hivyo watanzania mbalimbali waishio nchini humo wamepewa nafasi ya kushiiki kwenye mazishi hayo.
No comments:
Post a Comment