Huku
kukiwa bado hali si shwari ndani ya shirikisho la soka Ulimwenguni
FIFA, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Zico amepania
kugombea urais wa shirikisho hilo baada ya kukiri kufadhaishwa na janga
la rushwa katika uongozi wa FIFA.
Zico mwenye miaka 52 na ambaye
jina lake halisi ni Arthur Antunes Coimbra, amesema ni wajibu wake
kugombea. Akizungumza na kundi kubwa la waandishi wa habari katika kituo
chake cha kufundisha soka huko mjini Rio de Janerio, Zico amesema ni
huzuni kwaenye michezo kuona kile kinachotokea katika soka leo hii.Kuona
rushwa, lakini pia kuona uchapakazi unaofanywa na baadhi ya watu wazuri
ukipotezwa.Pia aliongeza kuwa, ni wajibu wake sasa kutumiauzoefu na
ujuzi wake kujaribu kugombea urais.Hivi karibuni rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter, alitangaza kuwa atajiuzuru wadhfa wake huo ikiwa ni siku nne tu baada ya kuchaguliwa tena kushika madaraka hayo. Uamuzi huo wa Blatter ulikuja ikiwa ni siku chache tu baada mamlaka ya Marekani na Uswiz kufungua kesi ya rushwa ya kwa baadhi ya maafisa FIFA.
No comments:
Post a Comment