Dk Kawambwa amekwenda chuoni hapo kwa lengo la kuzungumza na
uongozi wa chuo pamoja na wanafunzi kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi
suala hilo ambapo mbali na kukiri kuwa kuna taasisi ambayo
haikufanyakazi yake inavyopasa hadi hayo yakatokea amesema serikali
itatoa tamko juu ya hatma ya wanafunzi waliomaliza kozi hiyo na vyeti
vyao kutokutambuliwa kwenye ajira.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa TCU Prof Yunuth Mgaya amesema
bodi yake haihusiki na mgogoro huo na kwamba chuo hicho kimesajiliwa na
kipo nchini kisheria huku akiwatoa hofu wazazi wenye watoto wao chuoni
hapo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kikao cha waziri akiwemo waziri wa
elimu wa chuo hicho Answari Mnyonge amesema wanafunzi wako tayari
kurudi madarasani pale tu usajili utakapokamilika huku afisa habari wa
KIU akielezea athari zilizotokana na vurugu zilizotokea hivi karibuni
chuoni hapo.
Hata hivyo licha ya wanafunzi hao kutakiwa kuondoka chuoni hapo
baada kutangaziwa kuwa kimefungwa lakini bado wameendelea kuwepo
kushinikiza utatuzi wa mgogoro huo huku askari wa kikosi cha kituliza
ghasia FFU wakiendelea kuimarisha ulinzi chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment