Friday, 5 June 2015

Simba; Tuko tayari kumuuza singano kwenda Azam

Timu ya Azam FC ni moja kati ya klabu zinazowania saini ya kiungo huyo mwenye kasi ndani ya uwanja kwa ajili ya kumsajili katika usajili wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara
BAADA ya wa klabu ya Simba umesema upo tayari kumuuza kiungo wao mshambuliaji, Ramadhan Singano ‘Messi’ kwenye klabu ya Azam FC ambayo inasemekana ndiyo inamshawishi mchezaji huyo ili iweze kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.
Timu ya Azam FC ni moja kati ya klabu zinazowania saini ya kiungo huyo mwenye kasi ndani ya uwanja kwa ajili ya kumsajili katika usajili wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Msemaji wa Simba Haji Manara, ameiambia ukomboz blog kuwa wamepata taarifa hizo za mchezaji kufanya mazungumzo na Azam na hivyo wao wameona ni vyema wakamuachia mchezaji huyo aondoke kwa sababu tayari ameonekana ana mapenzi na klabu hiyo badala ya Simba.
“Tumegundua kuwa, katika sakata hili linaloendelea kati yetu na Messi zipo baadhi za timu zinahusika katika kumshawishi mchezaji huyo kwa kulazimisha kuwa mkataba umeisha wakati siyo ukweli sasa tunawataka Azam waje mezani tuzungumze kama kweli wanamtaka ‘Messi’ na pia wanatakiwa kujua kwamba kitendo cha kuzungumza na mchezaji huyo wakati bado anamkataba wa mwaka mmoja na Simba ni kosa la kisheria,”amesema Manara.
Manara amesema thamani ya Messi ni Tsh. Milioni 200 hivyo kama Azam wapo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa wanawakaribisha ili kuwenda kumaliza mzozo huo ambao umechukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari tangu uliopoanza wiki mbili zilizopita.
Post a Comment