Tuesday, 10 December 2013

Maelfu wakusanyika katika ibada ya kumuombea Mandela.

Mamia kwa maelfu ya waafrika Kusini na viongozi kiasi 100  wa dunia wamekusanyika katika uwanja wa soka wa Soweto mjini Johannesberg kwa ajili ya kushiriki ibada maalum ya kumuombea rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela.Pamoja na mvuwa inayonyesha,maelfu ya wananchi wanaendelea kumiminika katika uwanja huo wa mpira wakitokea sehemu mbali mbali za taifa hilo na duniani.Rais wa Marekani Barack Obama ni miongoni mwa viongozi watakaohutubia hadhara hiyo pamoja na makamu wa rais wa China Li Yuanchao , rais wa Cuba Raul Castro sambamba na rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na baadhi ya wajukuu wa Mandela.Sauti za watu wakiimba zinasikika kutoka uwanja huo uliofurika tangu mapema asubuhi ya leo.Baada ya kusaini kitabu cha rambirambi rais wa Urusi Vladmir Putin amemfananisha Nelson Mandela na Mahatma Gandhi na mpinzani wa kisovieti na mshindi wa tuzo ya Nobel mwandishi vitabu Alexander Solzhenitsyn akisema alikuwa ni mtu wa kutetea utu.Mandela atazikwa tarehe 15 Desemba katika kijiji cha Qunu.

No comments: