Monday, 23 November 2015

Wapinzani wachukua dola Argentina

Macri
Macri alikuwa ameshindwa kwenye duru ya kwanza

Mgombea wa chama cha upinzani cha Conservative Mauricio Macri amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais Argentina, huku mgombea wa chama tawala akikubali kushindwa.
Baada ya karibu kura zote kuhesabiwa, Bw Macri alikuwa na 52% akilinganishwa na Daniel Scioli aliyepata 48%.
Shangwe na vigelegele vilitanda katika makao makuu ya kampeni ya Bw Macri baada ya kura za maoni runingani kuonyesha alikuwa ameshinda.
Bw Macri, meya wa zamani wa Buenos Aires, alikuwa ameshindwa na Scioli, ambaye ni gavana wa mkoa wa Buenos Aires, kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi Oktoba.
Lakini wote wawili hawakuweza kushinda moja kwa moja na duru ya pili ikaandaliwa, mara ya kwanza kwa uchaguzi kuingia duru ya pili katika historia ya Argentina.
Ushindi wa Bw Macri ndio wa kwanza katika zaidi ya mwongo mmoja kwa upinzani wenye kuegemea siasa za mrengo wa kati kulia.

Saturday, 21 November 2015

Rais wa Mali atangaza hali ya Hatari

MaliWengi wa mateka waliokolewa
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza hali ya hatari nchini humo baada ya shambulio kwenye hoteli moja mjini Bamako kuua watu zaidi ya 20.
Bw keita ametangaza hali ya hatari itakayodumu kwa siku 10, pamoja na siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Watu wenye silaha wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Kiislamu walishambulia hoteli ya Radissom Blue mjini Bamako na kushikilia mateka watu 170.
Maafisa wa Marekani wamethibitisha hakuna mateka zaidi wanaoshikiliwa.
Makundi ya Al-Qaeda Afrika Kaskazini na kundi jingine la al-Murabitoun yamedai kuhusika kwenye shambulio hilo

Thursday, 19 November 2015

Nadal amchapa Andry Murray

Nadal amchapa Murray
Mchezaji namba tano kwa ubora wa mchezo wa tenesi kwa upande wa wanaume Rafael Nadal,amemshinda muingereza Andry Murray.
Nadal ameshinda mchezo huo kwa jumla ya seti 6-4 6-1, mchezo uliofanyika katika uwanja wa O2 Arena.
Nae Stan Wawrinka anayeshikilia nafasi ya nne kwa ubora alimfunga mpinzani wake David Ferrer aliyeko katika nafasi ya saba kwa jumla ya seti 7-5 6-2.
Murray atacheza na Wawrinka katika mchezo wa mwisho wa makundi siku ya ijumaa.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa amri kushikiliwa kwa afisa wa juu

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa amri kushikiliwa kwa afisa wa juu anayetuhumiwa kwa wizi wa zaidi ya dola bilioni mbili zilizotarajiwa kununua silaha za kukabiliana na wapiganaji wa Boko Haram.
Afisa huyo Sambo Dasuki alikuwa mshauri wa masuala ya usalama ya taifa kipindi cha utawala wa Rais aliyemaliza muda.

Wednesday, 18 November 2015

Rufaa ya Sepp Blatter na Platini yakataliwa


Sepp Blatter na Michel Platini
Maombi ya rais wa FIFA Sepp Blatter na makamu wa rais wa shirikisho hilo Michel Platini ya kupinga kusimamishwa kazi kwa siku 90 waliowekewa na kamati ya Fifa yamekataliwa.
Wawili hao walisimamishwa kazi mnamo mwezi Octoba huku kamati ya Fifa ikichunguza madai ya ufisadi dhidi yao.

Ufaransa yawaua wapiganaji 33 Syria

wapiganaji wa islamic state mjini Raqqa

Mashambulio ya Ufaransa na mataifa mengine dhidi ya ngome ya Islamic State huko Raqqa nchini Syria siku ya jumapili yamewauwa takriban wapiganaji 33,wanaharakati wamesema.
Kundi la wapiganaji wa haki za kibinaadamu kutoka Syria limesema kuwa wengi walifariki wakati vituo vya kukagua watu vilivyoshambuliwa.

Saturday, 14 November 2015

Anna Makinda aukimbia Uspika

Anna Makinda
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kumi, Anne Makinda ameamua kukaa kando ya mbio za Uspika wa Bunge la 11, siku chache baada ya kufanya kampeni kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa Mama Makinda aliamua kuchukua uamuzi huo wa kujiweka kando ya mchuano huo baada ya kushauriwa na watu wake wa karibu kufuatia dalili walizoziona kwenye mchakato huo pamoja na mambo mengine.

Awali mama Makinda alidaiwa kuanza kampeni kupitia ujumbe mfupi alioutuma kwa wabunge wateule kupitia simu za mkononi akiwapongea na kuwaomba kumuunga mkono kuwa Spika wa Bunge la 11.