Ilikuwa ni tafrani katika mtaa wa mianzini jijini hapa leo
wakati mradi wa utanuzi wa barabara kutoka mianzini kwenye mataa hadi ilding’a
ukiendelea, Tingatinga lililokuwa likifanya kazi ya kutanua barabara hiyo lilipochimbua
mfuko wa plastiki uliokuwa umesheheni
minoti ya hela uliokuwa
umechimbiwa chini kwenye nyumba moja ya matope iliyokuwa imebomolewa kupisha
utanuzi wa barabara hiyo.
Katika hali ya kushangaza jijini Arusha eneo la Mianzini
yamepatikana mamilioni ya hela yakiwa yamefukiwa chini ya Ardhini.
Katika eneo la tukio ilikuwa ni sherehe na vifijo kwa wapiti
njia waliokuwa wakijitafutia riziki lakini ilikuwa kilio kwa familia ya mzee
Christopher Akoonay alimaarufu kwa jina la “MBULU” ambaye inasemekana ni
mmiliki wa nyumba iliyobomolewa kupisha utanuzi wa barabara hiyo .
Akoonay hujishughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na
hufanya biashara ya kusambaza maziwa katika jiji la Arusha na viunga vyake,
Alizungumza na Mwandishi wetu kwa njia ya simu mzee Akoonay alitueleza “
Nikweli hela ni zangu na nyumba iliyobomolewa ni yangu “ alisema Akooney ,
hakuishia hapo aliendelea kusema anashangaa wajenzi wa barabara hiyo kubomoa
nyumba yake kwani yeye na baadhi ya wananchi walifungua shauri mahakamani kudai
fidia endapo nyumba zao zitabomolewa kabla ya mradi wa barabara kupita hapa”
lakini kesi ilitupiliwa mbali na mahakama , wajenzi hawakusubiri hata lisaa
walianza moja kwa kubomoa nyumba zetu hata nikiwa sijatoa baadhi ya vitu vyangu
ndani.
Christopher Akoonay alipoulizwa kwanini hakupenda kuweka
hela zake benki alisema “ nilikosa imani na benki maana wakati nikifanya kazi
kama mtumishi wa serikali miaka ya 1980 nilikuwa nina akaunti benki baada ya
kustaafu mwaka 1994 nikaamua kujishughulisha na shughuli za ufugaji
sikufuatilia akaunti yangu baada ya kustaafuhadi ilipofika mwaka 2000
nilikwenda kuangalia fedha zangu benki nikaambiwa kwasababu nimekaa zaidi ya
miaka 10 napaswa kwenda benki kuu kujieleza kwa nini sikutumia akaunti hiyo kwa
mda mrefu , nkaona huo ni usumbufu sikufuatilia na ndipo nilipopoteza imani na
benk na kuamua kujihifanyia fedha zangu nyumbani
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo walipo hojiwa na mwandishi
wetu , wakizungumzia swala hilo kwa masharti ya kutotajwa majina yao wamesema
wanashangazwa na Akoonay kuwa na kiasi kikubwa cha fedha kiasi kikubwa namna
hiyo na kuzifukia chini ya aridhi wakati anaishi kwenye nyumba ya matope.
No comments:
Post a Comment