Waziri wa mambo ya ndani nchini Mh. Mwigulu Nchemba aliwaagiza maafisa kuwasaka waalimu watatu wa mafunzo ambao wanadaiwa kumpiga mwanafuzi mmoja aliyefahamika kwa jina la Sebastian Chinguku anayesoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Mbeya day iliyoko jijini Mbeya.
mwalim Frank |
Walimu waliompiga mwanafunzi huyo walijulikana kwa majina
Mwalimu Sanke Gwanaka kutoka chuo kikuu
cha mwalimu Nyerere Memorial kilichoko Dar Es Salaam na Frank Msigwa , na john
Deogratius kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM). Inadaiwa waalimu hao
wakiwa katika mafunzo yao ya vitendo , mwalim Frank alitoa zoezi la somo la
kiingereza ambao baadhi ya wanafunzi walimgomea kufanya zoezi hilo akiwemo
mwanafunzi Sebastian. mwalimu huyo alianza kuwashambulia wanafunzi kwa viboko
ndipo Sebastian akahoji kwanini anapigwa , mwalimu alianza kumshambulia kwa
kumpiga makofi baadae alimpelaka staff room ( ofisin ) ambako waalimu walianza
kumshambulia kwa kumchapa na mwalimu Frank alianza kumpiga vibao na kumkaba koo
.
Tangu hapo baada ya mwanafunzi kuachiliwa alipotea shuleni na
kutokomea na waalimu hao walirudi vyuoni kwao.
Angalia video ya waalimu hao
wakimshambulia mwanafunzi huyo
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya ndani
Mh. Mwigulu Nchemba amedai uchunguzi wa awali unaonyesha tukio hilo lilitokea
mnamo tarehe 28 september 2016. Pia walimu wote wanaodaiwa kuhusika na tukio
hilo wanashikiliwa na jeshi la polisi , pia jeshi la polisi mkoani huko
wanaendelea kufanya mahojiano na uongozi wa shule ya sekondari Mbeya Day
No comments:
Post a Comment