Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulika
na utawala bora ya Tanzania Mzalendo Foundation, amesema nafasi
aliyofikia mama Salma akiwa mke wa rais mstaafu na ‘First Lady’ wa nchi
ni nafasi kubwa kiitifaki hivyo anapaswa kuwa na heshima na abakie kuwa
mama mshauri na mlezi wa taifa.
“Namuomba Mama Kikwete aige mfano wa mama Regina Lowassa
(mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa) ambaye wakati wa kampeni
za uchaguzi mkuu mwaka 2015 na baada ya uchaguzi Chadema ilimpa heshima
kwa kumteua kuwa Mbunge wa Viti Maalumu lakini kwa heshima aliikataa
nafasi hiyo.
“Mke wa rais mstaafu siyo mtu au kiongozi mdogo lazima
tujiulize inapotokea akachangia hoja ndani ya bunge ikapingwa au aambiwe
kaa chini au toka nje au atolewe nje na askari wa bunge je, hiyo
heshima au aibu na fedheha inaenda kwa nani?” amehoji Mgeja.
Pamoja na mambo mengine, Mgeja amesema wake wa viongozi ni
sehemu ya viongozi ambapo ana mashaka itifaki ndani bungeni inaweza
kugongana hivyo amemtaka Mama Salma Kikwete akapokea ushauri na mitazamo
ya watu mbalimbali na isimaanishe kwamba anamuonea wivu kwani maamuzi
yanabaki kwake kukataa ama kukubali ushauri huo kama changamoto katika
kupanga na kuchagua.
No comments:
Post a Comment