KAMATI ya Uongozi, Mipango na Fedha ya Baraza la Madiwani
la Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma, ilifunga Ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje ikidai ameshiNdwa kutekeleza
maelekezo ya madiwani.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dornart Nghwezi alisema
Mkurugenzi huyo na timu yake wamekuwa hawatekelezi kwa wakati maelekezo
ya Baraza hali inayosababisha kuwapo malumbano ya mara kwa mara
yanayokwamisha maendeleo.
Alisema wamewahi kutoa tamko la baraza la kutokuwa na imani
na mkurugenzi huyo kwa kushindwa kusimamia mapato na shughuli za
Halmashauri.
Aidha, alisema katika kikao cha Baraza la Madiwani
kilichofanyika Machi 16, mwaka huu, kikao cha Kamti ya Uongozi, Mipango
na Fedha walipanga kufanya kikao kingine Machi 27, lakini walipofika
ofisini hawakukuta makabrasha pamoja na uwepo wa kikao na walipojaribu
kumpigia simu, Mkurugenzi huyo hakupatikana.
Maje alikiri kuzuiwa kuingia ndani ya ofisi na madiwani hao
walioongeza kufuri lingine nje ya geti la nje la ofisi. Alisema hali
hiyo ilimlazimu kutoa taarifa Polisi na uongozi wa wilaya.
Maje alisema ni kweli walipanga kufanya kikao hicho Machi
27, lakini kikaathiriwa na ugeni wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uongozi
na Serikali za Mitaa ambao ulitaka kutembelea miradi mbalimbali ya
halmashauri hiyo.
“Ni kweli jana (juzi) kulitakiwa tuwe na kikao lakini kuna
ugeni wa Kamati ya Bunge ya kutembelea halmashauri yetu ikiwa ni pamoja
na wakuu wa idara wengi walitakiwa kwenda kwe ziara hiyo sasa hicho
kikao angekifanya nani? Tulimpa taarifa Mwenyekiti sasa sielewi kwanini
waliamua kufanya hivyo,” alisema Mkurugenzi huyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Wilaya
ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alisema kilichofanywa na madiwani hao
hakikuwa sahihi kwa kujaribu kumzuia kuingia ofisini.
Alisema kufunga milango ya ofis ni kitendo cha kijinai lazima taratibu, kanuni na sheria zifuatwe.
No comments:
Post a Comment