Saturday, 1 April 2017

TAARIFA TOKA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM

JAJI DYANSOBELA AMZUIA MSAJILI JAJI FRANCIS MUTUNGI KUTOA FEDHA ZA UMMA (RUZUKU YA CUF) KWA LIPUMBA NA KUNDI LAKE:
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
THE DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION
P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA UMMA
Imetolewa leo Tarehe 31/3/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa
JAJI DYANSOBELA AMZUIA MSAJILI KUTOA FEDHA ZA UMMA (RUZUKU) KWA LIPUMBA NA KUNDI LAKE:
MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM MBELE YA MHESHIMIWA JAJI DYANSOBELA katika Shauri No.  28/2017 leo Tarehe 31/03/2017 IMETOA AMRI DHIDI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI JAJI FRANCIS MUTUNGI KUMZUIA KUTOTOA FEDHA ZA RUZUKU YA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) MPAKA SHAURI NAMBA 21/2017 DHIDI YA MSAJILI NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUHUSU KUTOA FEDHA ZA RUZUKU SHILINGI MILIONI 369 KWA NJIA ZA WIZI NA UDANGANYIFU LITAKAPOSIKILIZWA NA KUTOLEWA MAAMUZI.
Amri hiyo ya Mahakama Kuu imekuja baada ya Jopo la Mawakili wasomi wa Chama wanaoiwakilisha Bodi ya Wadhamini ya CUF (THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRON (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) Mhe. Juma Nassor, Mhe Daimu Halfani na Hashim Mziray kuwasilisha maombi hayo mbele ya Mahakama Kuu kuiomba Mahakama Kuu kutoa Amri hiyo kwa kuwa fedha zilizotolewa awali Milioni 369 hazijulikani zimetumika vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa Chama –CUF juu ya fedha hizo ikizingatiwa kuwa Lipumba alishavuliwa Uanachama. Wakili Msomi Juma Nassor aliyewasilisha maombi hayo aliweka mkazo na kusisitiza kuwa kwa mazingira yaliyopo ni vyema na Busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama Ruzuku kwa Chama Cha CUF kwa sasa ZIENDELEE KUBAKIA SERIKALINI.  Aidha, Mawakili wasomi wameiomba Mahakama Kuu amri hiyo pia ifungamane na Kesi ya Msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya Msajili kumtambua Lipumba kwa Nafasi ya Uenyekiti iliyopo mbele ya Jaji Kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa Rufaa/maombi ya kufanyiwa Marejeo-REVISION mbele ya Mahakama ya Rufaa-Tanzania.
Mhe Jaji Dyansobela amekubaliana na Hoja zote hizo zilizowasilishwa kwa HATI YA DHARURA(UNDER CERTIFICATE OF URGENCY)  NA KUTOA AMRI YA KUZUIA FEDHA ZA SERIKALI KUTOLEWA KWA MASLAHI YA UMMA MPAKA HAPO MASHAURI YOTE YATAKAPOSIKILIZWA NA KUAMULIWA IPASAVYO.
Katika Hatua nyingine ili kuhakikisha kuwa masuala ya kesi yote yanasimamiwa na kushughulikiwa na kumalizwa kwa haraka Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad ameshakamilisha mazungumzo ya kuongeza nguvu zaidi za utetezi wa kisheria kwa kuwapata Mawakili Wasomi Maarufu sana nchini watano (5) ambao wataungana na kutengeneza jopo la Mawakili 9 watakaosimamia Kesi zote dhidi ya Lipumba na kundi lake.
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
----------------------------------------------
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA- CUF TAIFA
MAWASILIANO: 0784 001 408/0715 062577

No comments: