Msanii kutoka Ufaransa Abraham Poincheval anaendelea
kuatamia mayai ya kuku akiwa na matumaini kwamba mwishowe yataangua
vifaranga.
Msanii huyo anatumia joto kutoka kwa mwili wake kutamia mayao hayo 10.
Poincheval ambaye hufanya uigizaji wa kuigiza mambo ya
ucheshi lakini ya hatari tayari ameishi wiki mbili ndani ya dubu,
miongoni mwa mambo mengine ya kushangaza.
Atakuwa katika chumba maalum ambacho anatamia mayai, ambapo
watalii wanaweza kumtazama katka makumbusho ya Palais de Tokyo mjini
Paris.
Anatarajia kutamia mayai hayo kwa siku 21 hadi 26.
No comments:
Post a Comment