Vilabu vitatu vya Ligi ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga
vinamfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana
Samatta.
Kwa mujibu wa wakala anayeishi Ubelgiji makachero wa timu za
Wolfsburg, Hamburger SV na Borussia Mönchengladbach wamekuwa
wakimfuatilia Samatta anayetajwa kuwekewa thamani ya euro milioni 10.
Klabu ya Genk inasemekana iko tayari kumuachi Samatta mwenye mkataba
hadi mwaka 2020 kwa dau lisilopungua euro milioni 10 licha ya kumnunua
kwa Euro 800,000 kutoka klabu ya TP Mazembe mwanzoni mwa mwaka jana.
No comments:
Post a Comment