Mshambuliaji wa Atletical Madrid aliyehusishwa kwa mda mrefu kuhamia Klabu ya Manchester United Antoine Griezman amewakatisha tamaa mashabiki wa man u baada ya kuandika katika akaunti yake ya twitter kuwa bado anafurahia kubaki A.Madrid na taarifa zinazomhusisha na kutaka kuhama ni za uongo zipuuzwe.

bu hiyo kwa ada ya uhamisho wa £6 million.
Manchester city wamewapiku jirani zao Manchester United kwa kumfanikisha kupata saini ya mchezaji wa Monaco Bernardo Silva kwa kiwango cha £43million . Huku klabu ya napoli ikifanikiwa kumbakiza mchezaji wake mahiri Dries Mertens ambaye mkataba wake ulikuwa unakaribia kufika kikomo , Dries Mertens ameingia mkataba mpya na klabu yake hadi 2022.

Klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa imeingia kwenye vita kali na klub ya newcastal katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anamtolea macho mchezaji wa kimataifa wa Ujermani na klabu ya Borussia Dortmund Mario Gotze ili kuziba pengo la mshambuliaji wake Philippe Coutinho
anaetazamiwa kujiunga na miamba wa soka nchini Uhispania Barcelona.
Katika hali ya sintofahamu wamiliki wa Arsenal juzi walikuwa wamemwahidi kocha wa Arsenal arsen wenger kuwa atapatiwa mkataba wa miaka miwili endapo watapata matokeo mazuri dhidi ya chelsea katika fainali ya kombe la FA , hata hivyo Wenger haku chezea bahati hiyo alifanikiwa kutwaa kombe la FA kwa kuwachapa Chelsea 2-1 , hivyo inatazamiwa wenger akaongezewa mkataba wa miaka miwili