Baadhi ya Mawakili jijini Kigali wamekosoa kitendo cha
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam cha kumkamata rais wa
chama cha wanasheria Tundu Lissu ambaye alikuwa njiani kuelekea jijini
humo kuhudhuria mkutano.
Tundu Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),
amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha
Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.
”Huu ni mpango wa kumdhoofisha, kwanini asingekamatwa
jana?” amehoji wakili wa kujitegemea Rwebangiza Kiondo kutoka Tanzania,
ambaye yupo jijini humo kwa shughuli za kufuatilia uchaguzi wa Rwanda.
Wakili Rwebangiza ameiambia BBC, kuwa Polisi wanatumia
nguvu nyingi kupambana na Mwanasheria huyo ambaye alikuwa akitekeleza
majukumu yake.
”Unamkamata Wakili akiwa katika pilika za kutekeleza wajibu
wake, tena kwa kumshtukiza utafikiri ni jambazi anayetafuta, sikatai
kwamba huenda pana hoja lakini kwanini umshtukize, mtu ambaye ni
mbunge?”