Wednesday, 6 January 2016

Korea Kaskazini yafanya jaribio la bomu

Kiongozi wa Korea KaskaziniKim Jong Un kiongozi wa Korea Kaskazini
Korea Kaskazini inasema kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la nguvu ya maji, maarufu kama bomu la haidrojeni.
Tangazo hili limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya ardhi ya kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia. Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikua majaribio ya bomu hilo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu.

 
Kiongozi wa Korea KaskaziniTangazo hilo lilitolewa na runinga ya taifa
Mwandishi wa BBC anasema bomu la nguvu ya maji lina uwezo mkubwa wa mlipuko ikilinganishwa na mabomu mengine yenye madini ya Plutonia ambayo Korea kaskazini imefanya majaribio katika miaka ya awali.
Mamkala za Pyongyang zimefanyia majaribio mengine matatu ya kinyukilia katika eneo kulikofanywa majaribio ya sasa kwa kipindi cha miaka kumi

Mbwana Ally Samatta atua Nigeria sherehe za kutuza wachezaji

Mbwana Samatta
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta leo hii anatarajiwa kuwasili nchini Nigeria kuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora barani Afrika zitakazofanyika katika mji wa Abuja Alhamisi tarehe 7 Januari.
Mbwana Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAF CL) baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao 8 na kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.
Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameandamana na Samatta kuhudhuria sherehe hizo.

Monday, 4 January 2016

TETESI ZA SOKA ULAYA

Manchester United wanajiandaa kutoa pauni milioni 140, ili kutengua kigezo cha uhamisho cha Neymar, 23 anayeichezea Barcelona, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua (Le Sport10), Manchester United watamruhusu kiungo wao Nick Powell, 21 kwenda kwa mkopo katika timu moja ya ligi daraja la kwanza (Sun), Southampton hawatomuuza Sadio Mane, 23 au Victor Wanyama, 24 katika dirisha la usajili ya Januari (Times),

Watu 8 Wakiwemo Polisi Wafariki Dunia Kwa Kusombwa na Maji Kibaigwa Mkoani Dodoma



WATU 8 wamefariki dunia katika ajali iliyosababishwa na gari kusombwa na maji huku watu 6 wakiwa wa  familia moja.

 Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Davidi Misime amesema majira ya saa tatu usiku Jumapili, wananchi wa Kibaigwa walitoa taarifa jeshi la polisi kwa madai kwamba kuna gari limesombwa na maji na limetumbukia katika mkondo wa maji.

Shilole ajuta kuchora tatuu za Mziwanda kifuani kwake

Shilole ameapa kutorudia tena kuchora tattoo yenye jina la mpenzi wake.
Hivi karibuni muimbaji huyo alilazimika kuifuta tattoo ya jina la aliyekuwa mpenzi wake, Nuh Mziwanda.
Shilole amesema kujichora tattoo ya jila Nuh kumemharibia issue kibao.
“Tattoo hapa ni empty,” aliambia 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii.

Saturday, 2 January 2016

Mhubiri wa Kishia anyongwa Saudi Arabia

Sheikh Nimr al-NimrFamilia ya Sheikh Nimr al-Nimr inasema maandamano yake yalikuwa ya amani
Saudi Arabia imemuua mhubiri maarufu wa dhehebu la Kishia Sheikh Nimr al-Nimr, wizara ya masuala ya ndani imesema.
Mhubiri huyo ni miongoni mwa watu 47 waliouawa baada ya kupatikana na makosa yanayohusiana na ugaidi, imesema kupitia taarifa.
Sheikh Nimr aliunga mkono sana maandamano dhidi ya serikali yaliyochipuka mkoa wa Mashariki mwaka 2011, ambako Washia walio wengi walilalamikia kutengwa.

Friday, 1 January 2016

Magari ya kibinafsi kuzuiwa kuingia Delhi

DelhiMagari ya kibinafsi yamekuwa yakiongezeka sana Delhi
Wasimamizi wa mji mkuu wa India, Delhi wameanza kuzuia baadhi ya magari ya kibinafsi kuingia mjini ili kupunguza uchafuzi wa hewa.
Magari ya kibinafsi yenye nambari za usajili zinayogawika na mbili bila masalio (namba shufwa) na yale yenye nambari zisizogawika na mbili (namba witiri) zitakuwa zikiruhusiwa mjini siku tofauti.
Mpango huo utafanyiwa majaribio kwa kipindi cha wiki mbili, na unatarajiwa kuzuia magari milioni moja kuingia mjini kila siku.