Korea Kaskazini
inasema kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufanya majaribio ya bomu la
nguvu ya maji, maarufu kama bomu la haidrojeni.
Tangazo hili
limetolewa na runinga ya taifa baada ya kusikika mitetemeko ya ardhi ya
kipimo cha tano nukta moja, karibu na eneo kuliko na kinu cha nyukilia.
Wataalamu wa Marekani wanafanya uchunguzi ikiwa yalikua majaribio ya
bomu hilo au ilikua zana nyingine ya nyuklia isiyokuwa na nguvu.Mamkala za Pyongyang zimefanyia majaribio mengine matatu ya kinyukilia katika eneo kulikofanywa majaribio ya sasa kwa kipindi cha miaka kumi
Manchester United wanajiandaa kutoa pauni milioni 140, ili kutengua
kigezo cha uhamisho cha Neymar, 23 anayeichezea Barcelona, baada ya
mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua (Le Sport10), Manchester United
watamruhusu kiungo wao Nick Powell, 21 kwenda kwa mkopo katika timu moja
ya ligi daraja la kwanza (Sun), Southampton hawatomuuza Sadio Mane, 23
au Victor Wanyama, 24 katika dirisha la usajili ya Januari (Times),
