Thursday, 31 August 2017

Je Mahrez atajiunga na timu gani ? soma hapa

Riyad Mahrez ameruhusiwa kuondoka katika kambi ya kikosi cha Algeria na kurudi Ulaya ili kukamilisha uhamisho wake hadi klabu mpya kulingana na shirikisho la soka nchini Algeria.
Winga huyo wa Leicester aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka katika uwanja wa King Power na amehusishwa na vilabu vingi huku Roma ikiwa tayari imewasilisha ombi la kumununua mchezaji huyo mara tatu , ombi la mwisho likiwa lile la dau la £32m.

Monday, 14 August 2017

Waziri Mkuu aagiza wananchi wasizuiwe kuonyesha mabango

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka mabango yanayoonyeshwa na wananchi kwa viongozi wa kitaifa wanapowatembelea yasiwe yanazuiwa kwa vile yanakuwa yanaelezea changamoto wanazokabiliana nazo.

Majaliwa alisema hayo baada ya kuona mabango yaliyoinuliwa na wananchi kwenye mkutano wake na wananchi mwishoni mwa juma lililopita mjini Sikonge mkoani Tabora huku wananchi hao wakitakiwa kuyashusha.
“Siku nyingine msirudie na kuanzia sasa waacheni wananchi waonyeshe mabango yao kwani ndiyo njia wanayotumia kuonyesha hisia zao kwa yale wanayokumbana nayo na kuwasababishia kero,” alisema Majaliwa.

Friday, 21 July 2017

Mawakili Kigali walaani kukamatwa Rais wa wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu

Baadhi ya Mawakili jijini Kigali wamekosoa kitendo cha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam cha kumkamata rais wa chama cha wanasheria Tundu Lissu ambaye alikuwa njiani kuelekea jijini humo kuhudhuria mkutano.
Tundu Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)  akielekea Kigali, Rwanda  kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.
”Huu ni mpango wa kumdhoofisha, kwanini asingekamatwa jana?” amehoji wakili wa kujitegemea Rwebangiza Kiondo kutoka Tanzania, ambaye yupo jijini humo kwa shughuli za kufuatilia uchaguzi wa Rwanda.
Wakili Rwebangiza ameiambia BBC, kuwa Polisi wanatumia nguvu nyingi kupambana na Mwanasheria huyo ambaye alikuwa akitekeleza majukumu yake.
”Unamkamata Wakili akiwa katika pilika za kutekeleza wajibu wake, tena kwa kumshtukiza utafikiri ni jambazi anayetafuta, sikatai kwamba huenda pana hoja lakini kwanini umshtukize, mtu ambaye ni mbunge?”

magazeti ya leo tarehe 21.7.2017


Monday, 17 July 2017

TETESI ZA USAJILI LEO TAREHE 17/7/2017

Kulingana na gazeti la Sky Sports Klabu ya chelsea inataka kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang , katika harakati hizo chelsea imeongeza dau lake kutoka paundi milion 65 hadi kufikia paundi ilion 70 kuhakikisha wanapata saini ya mchezaji huyo baada ya kumkosa Romeu Lukaku aliyetua Man U .

Thursday, 13 July 2017

Ajira mpya 10,184 kuziba waliachishwa kazi kwa vyeti feki

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki
OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza kutoa vibali vya ajira 10,184 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais, Utumishi, Florence Temba, ilieleza kuwa agizo hilo linazihusu Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala wa Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma.
Ilimnukuu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akitoa agizo hilo wakati akizungumza katika kikao kazi na watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam jana.
“Mgawanyo wa vibali vya ajira umezingatia upungufu uliojitokeza baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki, vipaumbele vya Taifa kwa sasa na upatikanaji wa watumishi kutoka katika soko la ajira,” alisema Kairuki.

Wednesday, 12 July 2017

Tetesi za usajili leo tarehe 12.7.2017



Klabu ya Chelsea iliyo na maskani yake jiji la London imetuma ofa ya paund million 65 kwaajili ya kumsajili mshmbuliaji wa Borusia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gaboni.
Meneja wa Chelsea Antoni Conte ametuma ofa hiyo baada ya kukosa saini ya aliyekuwa mchezaji wa Everton Romeo Lukaku ambaye sasa amejiunga na mahasimu wao Manchester United jumatatu ya wiki hii. Mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo uekuja baada ya Chelsea chini ya meneja wake Conte kuonekana hana mpango na Diego Costa kwa msimu ujao ,Kwa Upande wa Dortmund wamefungua milango kwa mchezaji huyo kuuzwa , ripoti kutoka gazeti la “The Sun ” zineleza kuwa Pierre-Emerick Aubameyang anatamani sana kucheza ligi ya Uingereza. Aubemeyang aliibuka mpachikaji bora wa magoli katika ligi ya ujerumani msimu wa 2016/17, PSG na AC MILLAN pia zinafuatilia saini ya mchezaji huo kwa karibu zaidi