Sunday 8 May 2016

SAMIA : Ukawa wananguvu kuliko wabunge wa Ccm

HATIMAYE Mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) umekiri kwamba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekomaa.

Samia Suluhu Hasani, Makamu wa Rais wa Serikali inayoundwa na CCM amesema, upinzani una nguvu kubwa nchini na wabunge wa upinzani wamekomaa zaidi ya wa CCM.Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati wa ufunguzi mkutano wa UWT unaofanyika mjini humo katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu. Akifungua mkutano huo Samia amesema, kwa miaka 20 upinzani umezalisha wabunge waliopevuka na kwamba, ni lazima umoja huo ujiuliza, je wao wanawafundisha nini wabunge wapya wa Viti Maalum ambao wapo bungeni mpaka wanakomaa?

Mbali na hilo amesema, serikali kwa sasa inatakiwa kujiuliza, ni kwa namna gani itawakomboa akina mama ambao wapo katika mazingira magumu wakikabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama huku wakitembea umbali mrefu kufuata maji.

“Je Wabunge wa Viti Maalum ambao ni wapya mnawafundisha nini wanapokuwa bungeni wakitekeleza majukumu yao? Je, waendelee kujibu na kupiga vijembe au waweze kujenga hoja na kupenyeza bungeni matakwa na mahitaji ya wanawake wenzao?” alihoji.

No comments: