Luyima alikuwa ameshtakiwa pamoja na washukiwa wengine 12 kuhusiana na mashambulio hayo yaliyosababisha vifo vya watu 74.
Kundi la Kiislamu la al-Shabab kutoka Somalia lilidai kuhusika.
Jaji Alfonse Owinyi Dollo awali alikuwa ameamua kwamba washukiwa wote hawana hatia ya kuwa wanachama wa kundi la kigaidi kwa kuwa kundi la al-Shabab, halikuwa limeorodheshwa kuwa kundi la kigaidi mwaka 2010.
Mahakama bado haijatoa uamuzi kuhusu makosa hayo mengine yanayowakabili washukiwa hao ambayo ni pamoja na mauaji na kusaidia ugaidi.
No comments:
Post a Comment