Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani.
Klabu
hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika
mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200.Mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina alifunga mabao 18.
Rais wa Indi Native Diego Culequi amesema matokeo hayo hayakutarajiwa na wachezaji hawakuwa wamezoea joto kali ambalo anasema lilichangia kushindwa kwao.
Mwandishi wa habari Mwingereza Tim Vickery, ambaye amekuwa Brazil kwa miaka 20, amesema Bon Accord kwa sasa wamejadiliwa sana katika vyombo vya habari Ecuador.
Anasema ligi ya daraja la tatu ya Ecuador huwa na ushindani mkubwa.
Rekodi ya sasa inashikiliwa na Arbroath FC ya Scotland iliyofunga mabao 36-0 dhidi ya Bon Accord miaka 131 iliyopita.
Mwenyekiti wa Arbroath FC John Christison amesema ana wasiwasi kiasi kwamba rekodi yao waliyoiweka 1885 huenda ikavunjwa.
Amesema klabu hiyo itasubiri uamuzi wa Guinness World Records.
"Tutasikitika sana kama klabu iwapo tutaipoteza rekodi hii ambayo kama jiji twajivunia sana.
“Ilifahamika sana kwamba wakati huo kipa wetu hata hakugusa mpira na alisimama kwenye goli na mwavuli kwani mvua kubwa ilikuwa inanyesha.
"Lakini tutasubiri uamuzi wa maafisa wa Guinness.”
Siku hiyo ya ushindi wa Arbroath mwaka 1885, Dundee Harp walilaza Aberdeen Rovers 35-0.
Ingawa mwamuzi alisema mabao yalikuwa 37, karibu wa Dundee Harp alisema alirekodi 35 pekee, mabao ambayo mwishowe yalitambuliwa.
Mwaka 2002, mechi ya ligi kuu ya Madagascar ilitoa matokeo ya kushangaza baada ya mabingwa wateule AS Adema kulaza mahasimu wao wa jadi Stade Olympique I'Emyrne 149-0. Wachezaji wa Olympique walijifunga makusudi kwa hasira kulalamikia uamuzi wa refa.
Matokeo ya mechi hiyo hayakutambuliwa kimataifa.
No comments:
Post a Comment