Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatarajiwa
kutawazwa leo Ijumaa, siku tatu baada ya mtangulizi wake Robert Mugabe kuachia
ngazi kwa shinikizo la jeshi na chama chake cha Zanu-PF.
Aliyekua makamu wa rais anamrithi Mugabe, baada ya uhasama kati yake na mkewe Mugabe, Grace Mugabe, kutokea na kusababisha kufutwa kazi na kukimbilia nchini Afrika Kusini.
Grace Mugabe alitaka kumrithi mumewe, baada ya kukalia kiti cha makamu wa rais wa Zimbabwe.
Bw. Emmerson alirejea siku ya Jumatano jioni, siku moja tu baada ya mtangulizi wake kujiuzulu.

Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .
Upinzani unamtaka Emmerson Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi".
Vyombo vya habari vya serikali vimesema kuwa Robert Mugabe atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Bw. Munangagwa.
Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa michezo mjini Harare, huku waandalizi wakiwataka wa Zimbabwe kuhudhuria kwa wingi sherehe hizo.
UNAWEZA KUANGALIA HAPA NAMNA SWALA KA KUAPISHWA KWA RAIS WA ZIMBABWE LINAVYOENDELEA
👇👇👇👇👇👇👇👇👇