Thursday, 3 November 2016

Mawaziri wavutwa mashati bungeni

Image result for mipango waziriBunge la Jamhuri ya Muungano jana liliweka kando tofauti zao za kisiasa wakati lilipowaweka kwenye kibano mawaziri watano kutokana na utendaji wao.
Wabunge wa chama tawala na upinzani walionyesha makali yao wakijadili Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/18 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Serikali ya Rais John Magufuli iingie madarakani.
Mbali na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, mawaziri wengine waliowekwa kwenye hali ngumu ni Ummy Mwalimu, ambaye ni Waziri wa Afya, Angellah Kairuki (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi), Charles Mwijage (Viwanda, Biashara na Uwezeshaji) na Profesa Joyce Ndalichako (Elimu, Sayansi na Teknolojia)

Thursday, 6 October 2016

Walimu waliokuwa mazoezini waliomchapa mwanafunzi watiwa mbaroni.



Waziri wa mambo ya ndani nchini Mh. Mwigulu Nchemba aliwaagiza maafisa kuwasaka waalimu watatu wa mafunzo ambao wanadaiwa kumpiga mwanafuzi mmoja aliyefahamika kwa jina la Sebastian Chinguku anayesoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Mbeya day iliyoko jijini Mbeya.

Tuesday, 4 October 2016

Angalia alichokipost ROMA kuhusu birthday ya mwanae

Kuelekea birthday ya mtoto wa masanii wa HIPHOP nchini Tanzania ROMA aliposti  katika mtandao wa kijamii facebook akimtaka mwanae ampe ruhusa ya kuachia wimbo wake mpya

Baada ya kufungiwa kutumia uwanja wa taifa yanga yaandika barua kwenda TFF




Timu ya soka ya yanga imeandika barua kwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kuomba watumie uwanja wa Amaan Zanzibar kwa mashindano mbalimbali kama uwanja wa nyumbani.

mamilion ya pesa yakutwa yamechimbiwa chini Arusha



Image result for tanzanian shillingIlikuwa ni tafrani katika mtaa wa mianzini jijini hapa leo wakati mradi wa utanuzi wa barabara kutoka mianzini kwenye mataa hadi ilding’a ukiendelea, Tingatinga lililokuwa likifanya kazi ya kutanua barabara hiyo lilipochimbua mfuko wa plastiki uliokuwa umesheheni  minoti ya hela  uliokuwa umechimbiwa chini kwenye nyumba moja ya matope iliyokuwa imebomolewa kupisha utanuzi wa barabara hiyo.

Thursday, 29 September 2016

Raia wa Uganda Alfred Olango auawa na polisi Marekani

El CajonPolisi wamekiri kwamba Olango hakuwa na silaha
Polisi katika jimbo la California, Marekani wanasema wamemuua kwa kumpiga risasi mkimbizi wa Uganda ambaye wanasema alitoa kifaa chenye ncha kali mfukoni na kuwalekezea maafisa "kana kwamba alikuwa anawafyatulia risasi."
Baadaye, imebainika kwamba ilikuwa ni sigara ya kisasa ifahamikayo kama 'e-cigarette'.
Waandamanaji kadha wamejitokeza katika barabara za El Cajon, viungani mwa mji wa San Diego, kulalamikia kuuawa kwa Alfred Okwera Olanfo, aliyekuwa na umri wa miaka 38.
Bw Olango aliuawa Jumanne baada ya polisi kujibu wito kutoka kwa dadake Olanfo ambaye aliitisha msaada.

Arsenal yainyuka 2-0 Basel,

ArsenalTheo Walcott
Michuano ya klab bingwa barani ulaya inaendelea katika hatua ya makundi ambapo Usiku wa kuamkia leo michezo michezo nane ilipigwa katika viwanja tofauti.
Arsenal ikiwa nyumbani ilibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Basel ya nchini uswizi, magoli yote yaliwekwa kimyani na Theo Walcott.
PSG ikiwa ugenini iliibuka na ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.
Besiktas imeenda sare ya 1-1 dhidi ya Dynamo Kyiv. Huku SSC Napoli ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Benfica.
Borussia Moenchengladbach nayo ikiwa nyumabi imekubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Barcelona. Na mchezo wa kushangaza wa funga nikufunge ulikuwa kati ya Celtic na Manchester City, ambazo zilienda sare ya 3-3.
Atletico Madrid nayo ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Bayern Munich. Na FC Rostov ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya PSV Eindhoven