Pulido, anayechezea klabu ya soka ya Olympiakos ya Ugiriki alijikata mkono wake wakati akijaribu kuvunja kioo kwenye mlango ili atoroke kabla ya polisi kuwasili katika eneo hilo.Alitekwa siku ya jumamosi na watu waliokuwa wamefunika nyuso zao wakati akitokea kwenye sherehe moja karibu na mji wake anaoishi wa Ciudad Victoria katika jimbo la Tamaulipas.
Tuesday, 31 May 2016
Hivi ndivyo alivyookolewa Alan Pulido
Pulido, anayechezea klabu ya soka ya Olympiakos ya Ugiriki alijikata mkono wake wakati akijaribu kuvunja kioo kwenye mlango ili atoroke kabla ya polisi kuwasili katika eneo hilo.Alitekwa siku ya jumamosi na watu waliokuwa wamefunika nyuso zao wakati akitokea kwenye sherehe moja karibu na mji wake anaoishi wa Ciudad Victoria katika jimbo la Tamaulipas.
Samatta aiongoza timu yake kucheza Europa
Mshambuliaji wa
kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kufuzu kucheza
Ligi ya Europa baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5-1 na
kushinda kwa jumla ya mabao 5-3.
Kulingana na gazeti la
Mwananchi, Samatta, ambaye katika mchezo wa kwanza walionyukwa 2-0
alianzia benchi, jana aliaminiwa kuanza mchezo huo na kocha wake Peter
Maes, akicheza pamoja na Nikos Karelis katika safu ya bora ya
ushambuliaji.Katika mchezo huo, Samatta alifunga bao moja na kutegeneza mengine mawili yaliyofungwa na Karelis ambaye alifunga magoli matatu katika mchezo huo, na Sandy Walsh akifunga bao moja kabla ya Sporting Charleroi kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Jeremy Perbet.
Kulingana na Mwananchi,Genk, ikicheza kwenye uga wake wa nyumbani wa Cristal Arena ilianza mchezo kwa kasi na dakika 16, ilipata penalti baada ya Samatta kuangushwa kwenye eneo la hatari na kipa Nicolas Penneteau, ambaye alipewa kadi nyekundu
Monday, 30 May 2016
Kauli ya JPM kujitoa sadaka yazua mjadala
Kauli ya Rais John Magufuli kwamba yuko tayari kuutoa mwili wake sadaka katika kupambana na rushwa na ufisadi uku kuwasaidia wanyonge, imeibua mjadala huku wanasiasa wakitofautiana.
Akizungumza katika Mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema: “Unapoona watu wanashangaashangaa sana (ni) kwa sababu hawakuzoea haya. Na walifikiri nitakuwa part of them (sehemu yao), never (haitatokea), not me (si mimi).
“Ni mara 10 nisiwe rais, nikachunge hata ndege, nikakae kijijini kuliko niwe Rais halafu nivumilie uozo huu unaofanyika. I’m saying never (nasema haitatokea).”
Rais Magufuli amekuwa akizitoa kauli kama hizo mara kwa mara, hasa anapowawajibisha baadhi ya watendaji wa Serikali, huku ikidaiwa kuna upinzani mkali ndani ya chama chake cha CCM, hali inayohisiwa kusababisha kauli hiyo.
Mkurugenzi wa Fordia, Bubelwa Kaiza alisema kauli hizo za Rais Magufuli zinaonyesha uzalendo wa kweli na amefanikiwa kufanya mambo yaliyowashinda marais waliomtangulia.
“Ndani ya CCM kuna upinzani mkali kutoka kwa makada. Kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita watendaji wa Serikali wamekuwa na mikakati ya kusaidia wezi na utapeli, hivyo anachofanya ni ‘revival strategy (mkakati wa kufufua),” alisema Kaiza.
Mpatanishi mkuu wa muungano wa upinzani nchini Syria amejiuzulu
Mpatanishi mkuu wa
muungano wa upinzani nchini Syria amejiuzulu katika kile anachosema
kuwa, kuvunjika kwa mazungumzo ya amani, yenye nia ya kumaliza vita vya
wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka mitano sasa.
Mohammad
Alloush, anayetoka kwenye kamati kuu ya upatanishi HNC, amesema kuwa
anajiondoa kwa sababu mazungumzo hayo yanayoungwa mkono na Umoja wa
mataifa huko Geneva, hayajazaa matunda au kutanzua matatizo wanayopitia
raia wa Syria waliozingirwa na vita.Kamati kuu ya mazungumzo hayo ya amani iliahirisha shughuli zake mwezi Aprili na hakuna tarehe ambayo imewekwa ya kurejelewa kwa mazungumzo.
Thursday, 26 May 2016
Watanzania 8 waliotaka kujiunga na al-Shabab wakamatwa
Serikali ya Kenya
imefichua kwamba imewakamata raia wanane wa Tanzania waliokuwa katika
harakati za kujiunga na kundi la wapiganaji la al-Shabab nchini Somalia.
Katika
taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari, polisi wanasema raia hao
waliokamatwa katika kipindi cha miezi miwili iliopita walikiri kuwa
mbioni kujiunga na kundi hilo la ugaidi.Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya kundi la watu wanaojidai kuwa wapiganaji wa Kiislamu kuweka video mtandaoni likidai uwepo wa wapiganaji wa Kiislamu nchini Tanzania
Video hiyo iliwaonyesha wanaume hao wakiwa wamejifunika nyuso zao kwa vitambaa na barakoa.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na kuwahimiza Waislamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga na kampeni yao.
Klabu ya soka yafungwa mabao 44 Ecuador, Mchezaji afunga mabao 18 pekee
Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani.
Klabu
hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika
mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200.Mshukiwa wa ulipuaji Kampala apatikana na hatia
Luyima alikuwa ameshtakiwa pamoja na washukiwa wengine 12 kuhusiana na mashambulio hayo yaliyosababisha vifo vya watu 74.
Monday, 16 May 2016
Mikel Arteta kuondoka Arsenal
Nahodha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuhama klabu hiyo majira haya ya joto.
Arteta pamoja na kiungo wa kati mwenzake Tomas Rosicky wanatarajiwa kuondoka baada ya mikataba yao kumalizika.Sunday, 15 May 2016
Tisho la bomu laripotiwa Old Trafford
Mechi ya mwisho
katika ligi ya soka ya uingereza, EPL, kati ya Manchester united na
Bournemouth imeahairishwa kufuatia wasiwasi wa bomu, uwanjani Old
Trafford.
Kifurushi kinachoshukiwa kuwa na vilipuzi kilipatikana kimetegwa katika sehemu ya North West Quadrant.Wachezaji wakiongozwa na kocha Louis Van Gaal walirudi kwenye chumba cha mabadiliko.
Tayari kikosi cha timu hiyo kilikuwa kinajiandaa kuingia uwanjani baada ya kutajwa. Maelfu ya mashabiki waliokuwa wanasubiri mchuano huo walilazimika kutoka nje.
Saturday, 14 May 2016
Lady Jay Dee Sasa Kuitafuta Haki yake Kwa Njia ya Mahakama.

Friday, 13 May 2016
Serena William ala chakula cha mbwa
Nyota wa mchezo wa
tenisi kwa upande wa wanawake Serena Williams alijitia ugonjwa baada ya
kula chakula cha mbwa saa chache kabla ya kufuzu katika robo fainali ya
mashindano ya Italian Open.
Serena alijaribu kula kijiko kimoja
cha chakula cha mbwa wake kabla ya kumshinda Mmarekani mwenzake
Christina McHale katika seti za moja kwa moja.''Nilisema kwani kuna nini,nitajaribu kipande kimoja,kinaonja utamu'',alisema
Walimu walipwa vifaranga badala ya mshahara Uzbekistan
Mji mmoja nchini
Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala ya
pesa. Mamlaka za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la
Karakalpakstan wamekua wakitia vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na
uhaba wa pesa nchini humo.
Kituo cha radio kinachofadhiliwa na
Marekani{Radio Ozodlik} kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo
kama aibu kubwa kwa mamlaka.Zlatan Ibrahimovic kuondoka PSG
Mashambuliaji wa kiabu ya Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Kandarasi
ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 inakamilika msimu huu na
amehusishwa na uhamisho wa Manchester United,kilabu ya Los Angels Galaxy
na AC Milan.''Ninafurahia'',alisema.''Niliwasili kama mfalme na sasa naondoka kama kigogo lakini ntarudi''.
PSG imesema kuwa Ibrahimovic anaondoka kama mshambuliaji bora na mchezaji bora zaidi katika historia ya kilabu hiyo.
Ibrahimovic ameifungia mabao mengi zaidi klabu hiyo licha ya kujiunga nayo mwaka 2012 aiwa amefunga mabao 152 katika mechi 178.
PSG imeshinda taji la Ligue 1 kila msimu tangu Ibrahimovic ajiunge na kilabu hiyo.
Sunday, 8 May 2016
SAMIA : Ukawa wananguvu kuliko wabunge wa Ccm
HATIMAYE Mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) kutoka Chama Cha
Mapinduzi (CCM) umekiri kwamba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
imekomaa.
Samia Suluhu Hasani, Makamu wa Rais wa Serikali inayoundwa na CCM amesema, upinzani una nguvu kubwa nchini na wabunge wa upinzani wamekomaa zaidi ya wa CCM.Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati wa ufunguzi mkutano wa UWT unaofanyika mjini humo katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu.
Msichana Asiye na Mikono Ashinda tuzo la Muandiko Bora

Wakati anapoandika yeye husimama huku akishikilia kalamu yake katika mikono.
Mwalimu wake mkuu Tracy Cox kutoka shule ya Greenbrier Christian amemtaja kuwa mtu wa mfano mwema.
Akata sehemu za siri za mkewe ili apate mtaji

Mwanamke huyo anadai kujeruhiwa na mumewe usiku wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu akiwa wodini kwenye hospitali hiyo akiwa na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Siku ya tukio, nakumbuka mume wangu alikwenda kutembea, aliporejea nyumbani alifuatana na mtu mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji.“ Walipofika nyumbani aliniambia yupo na mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akitafuta viungo vya sehemu za siri za mwanamke akiwa na fedha milioni tano
Saturday, 7 May 2016
Mchezaji mwingine wa Cameroon afia uwanjani , Angalia VIDEO HAPA
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya soka barani Ulaya huenda utakuwa umekutana na taarifa za kusikitisha kwa taifa la Cameroon, usiku wa May 6 2016 Cameroon na Afrika kwa ujumla ilipata taarifa za kushtusha, baada ya kupokea taarifa za kifo cha kiungo wa kimataifa wa Cameroon aliyekuwa anaicheze Dinamo Bucuresti Patrick Ekeng.
Monday, 2 May 2016
Diamond Azipangua Shutuma za Kutoka na Mrembo Lyyn..Adai Wanajaribu Lakini Zari Ndio Roho yake

Diamond Ameamua Kuwakata watu vidomo wanaosema kuwa yeye na Zari kwa sasa hakuna mawasiliano mazuri kisa mrembo aliyecheza kwenye video mpya ya Rayvan...kwa kumpost Zari kwenye page yake ya Instagram...Tetesi za Diamond kutoka na msichana huyo zimekuwa gumzo kubwa instagram ....
Roho ya SIMBA!!!.... wanajaribu ila hawatokaa Waweze... Nakupenda Mpaka Naugua! @Zarithebosslady 😙 #Mmechelewa
Trump achekwa kwa alivyotamka Tanzania
Mgombea urais wa
chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya
kuonekana akiboronga akitamka Tanzania wakati wa kutoa hotuba.
Bw
Trump alikuwa akizungumzia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa katika
mabalozi ya Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 wakati wa
kuzungumzia sera yake ya kigeni.Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika akitamka ‘Tan-zay-nia’.
Binti wa Obama, Malia kusomea Havard
Mwanaye rais wa Marekani Barack Obama,Malia,amefuzu kujiunga na chuo kikuu cha Havard.
Taarifa
kutoka ikulu ya White House imesema kuwa Malia ambaye amekuwa
mapumzikoni baada ya kuhitimu masomo ya chuo cha upili, atajiunga na
chuo hicho cha kifahari mwakani.Malia ataendelea na likizo yake kabla ya kujiunga na Havard mwakani.'' taarifa hiyo ya ikulu ilielezea.
Magufuli apunguza kodi ya mapato na 2% kutoka 11% hadi 9%
Magufuli apunguza kodi ya mapato na 2% |
Huku wafanyikazi kote duniani wakiadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, nchini Tanzania, wafanyikazi wanakila sababu ya kutabasamu.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaongezea wafanyikazi wote nchini humo asilimia mia mbili 2% mishahara.Katika hotuba ya kuadhimisha siku ya wafanyikazi, bw Magufuli alitangaza kupunguzwa kwa kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11% hadi asilimia 9%.
Hii inamaanisha kuwa kila mfanyikazi atapata ongezeko la mapato yake kwa asilimia 2%.
Magufuli alitangaza kauli hiyo kufuatia ombi la wafanyikazi kupitia kwa katibu mkuu bwana Nicholus Mgaya la kutaka wanusuriwe makali ya mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu.
Subscribe to:
Posts (Atom)