Mchezaji kutoka Cameroon Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kurushiwa kitu na mashabiki katika mchezo wa ligi nchini Algeria.
Ebosse, 24, alithibitishwa kuwa amefariki baada ya kufikishwa hospitali katika eneo la Tizi Ouzou, mashariki mwa mji mkuu, Algiers.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya JS Kabylie, ambaye alikuwa amefunga goli moja katika mchezo huo waliopoteza kwa 2-1, dhidi ya USM Alger aligongwa na kitu hicho baada ya mpira kumalizika, wakati wachezaji wakiwa wanatoka uwanjani.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi imetaka uchunguzi kufanyika mara moja.
Haijathibitishwa ni kitu gani hasa alichogongwa nacho, lakini gazeti moja la Algeria limesema mashabiki walikuwa wamekasirishwa na kufungwa na walikuwa wakirusha mawe.
Taarifa iliyotolewa na klabu yake imesema :”alikufa kutokana na jeraha la kichwani” baada ya kurushiwa kitu mwisho wa mchezo.
Rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika, Issa Hayatou ametoa taarifa inayolaani tukio hilo
Timu ya taifa ya Zambia imepata
Kocha mpya, Honour Janza aliyechukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu
hiyo Patrice Beaumelle aliyeondoka mwanzoni mwa juma hili.
Rais wa Shirikisho la soka la Zambia Kalusha Bwalya amesema ni changamoto kubwa waliyonayo lakini wana imani na Janza.Zambia iko kundi F na itaikaribisha Msumbiji tarehe 6 mwezi Septemba, kisha itaelekea Cape Verde siku nne baada ya mechi hio.
Chipolopolo imefikia hatua ya kumtafuta mrithi wa Beaumelle baada ya mfaransa huyo kuamua kuungana na aliyekua kocha wa zambia Herve Renard ambaye kajiunga na Ivory Coast.
Bwalya amesema hana hofu kuwa Janza ambaye alikua Mkurugenzi wa ufundi ndani ya shirikisho la soka la zambia atamudu kuipeleka Zambia mbele.