Mwanafunzi anayesomea udaktari
nchini Marekani ambaye alikuwa ana nadi ubikra wake, amesitisha shughuli
hiyo baada ya watu wachache sana kujitokeza wakiwa tayari kuulipia
ubikra wa mwanamke huyo.
Pamoja na hilo Kern hakua na uhakika kuhusu ukweli wa waliojitokeza kulipia ubikra wake.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Daily Mail.
Mwanafunzi
huyo, Hanna Kern alikuwa ana nadi ubikra wake chini ya jina ambalo sio
lake 'Elizabeth Raine' kwa hofu ya watu kumtusi. Pia hakuweka sura yake
kwenye mtandao hadi alipofanya mahojiano na jarida la Haffington post.
Kern ana umri wa miaka 28 na ana digrii ya uzamifu kutoka chuo kikuu cha Washington, nchini Marekani.
Kern ni mwanafunzi wa hivi karibuni aliyenadi ubikra wake kwenye mtandao bila matokeo aliyoyataka.
Hata
hivyo alilazimika kuusitisha mnada wake baada ya kukosa kupata kima
alichokitaka na hata pia kukosa kupata wanaume wengi waliovutiwa na
kampeini yake na kuhofia kuwa waliojitokeza kuulipia sio watu wakweli.
Pia
alieleza kuwa alisumbuka sana kiakili kutokana na umaarfu aliopata
baada ya kufichua jina lake la kweli na kuonyesha sura yake.
Alikunukuliwa
akisema baada ya kukosa kufanikiwa kupata hela alizozitarajia, hana
wasiwasi na hilo kwani amapeta funzo na kujua kwa nini kampeini kama
hizi huwa kazifanikiwi.
Wa mwisho aliyejitokeza kulipia ubikra
wake alikuwa ametoa kima cha dola 801,000,lakini mwanafunzi huyo aliamua
kutoendelea na juhudi zake kwani hakufurahishwa na pesa hizo.
''Nimeamua kusitisha kempeini yangu, na kurejea katika msomo yangu ya udaktari.''
''Bado
ninaamini kuwa ubikra ni kitu kizuru na pia ninaamini kuwa mwanamke
anapaswa kuachwa afanye anavyotaka, '' ingawa kwa sasa masomo ndio
ninayotaka kushughulika nayo,'' alisema Kern.
Mshambuliaji matata wa kilabu ya Gor Mahia nchini Kenya Dan Sserenkuma aihama kilabu ya Simba SC
Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu ya Tanzania Simba SC.
Raia
huyo wa Uganda alijiunga na kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na
kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika ligi ya Kenya ambapo
alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga na Gor ambapo
alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.
''Nimefurahia
miaka miwili na nusu katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati
muhimu wa kuaga.Tumefurahia nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki
wamenisaidia sana hususan wakati mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi
katika ligi ya Kenya aliandika katika mtandao wake wa Twitter.
''Ningependa kumshukuru kila mtu katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.
Dan Sserenkuma
Mchezaji huyo wa kimataifa
katika timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katika mtandao wa kilabu
hiyo akifanyiwa majaribio pamoja na kupimwa afya na sasa anatarajiwa
kujiunga na wachezaji wenzake katika barabara ya Msimbazi mjini
Daresalaam tayari kwa maandalizi ya mechi za ligi ya Tanzania.
Wakati huohuo imebainika kwamba Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
Duru
zimearifu kuwa mchezaji huyo aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia
ripoti za vyombo vya habari kwamba alitarajiwa kujiunga na Simba.
Lakini
Gor Mahia haikuwasilisha ombi lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo
tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye thamani ya shilingi millioni 3
pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na kilabu hiyo ya Tanzania
ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia Mungai Kiongera.
Mahakama kuu nchini Zambia
imetangaza kuwa waziri wa Ulinzi Edgar Lungu ndio atakeyewania wadhfa wa
Urais kupitia tiketi ya chama cha Patriotic Front katika uchaguzi wa
mwezi Ujao.
Chama cha Patritic Front kimegawanyika kuhusu ni nani atakayekrithi rais sata kufuatia kifo chake.
Mgawanyiko huo utafungua njia kwa upinzani kuchukua mamlaka katika uchaguzi huo kulingana na wachambuzi.
Makundi
pinzani ya chama cha PF yalifanya mikutano tofauti katika kipindi cha
juma moja ili kumchagua mgombea wa urais katika uchaguzi huo wa january
20.
Upande wa bwana Lungu ulipinga uteuzi wa Bwana Sampa mahakamani.
''Mkutano
wa chama unaodaiwa kufanyika Disemba mosi ambapo mheshimiwa Miles sampa
anadaiwa kuchaguliwa kama mgombea wa chama cha Patritic Front nataka
kutangaza kwamba ni haramu na uamuzi wote ulioafikiwa si wa
halkali'',Jaji aliamuru.
Kaimu rais wa Zambia Guy Scott
Bwana sampa amesema kuwa atakataa rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Kiongozi
huyo ni mshirika wa karibu wa kaimu rais Guy Scott ambaye alichungua
mamlka baada ya kifo cha Sata katika hospitali ya Uingereza mnamo mwezi
Octoba akiwa na umri wa miaka 77.
Bwana Scott alichukua jukumu
muhimu katika mgogoro wa kuwania mamlaka alipomuondoa kwa mda bwana
Lungu kama katibu mkuu wa chama hicho mda mchache baada ya kifo cha
Sata.
Hatahivyo alilazimika kurudisha bwana Lungu siku moja baadaye kufuatia lalama katika chama.
Bwana Scott ambaye hawezi kupigania urais anajaribu kuwa mtu muhimu katika siasa za taifa hilo kulingana na wachambuzi..
Mama wa kijana anayeugua kifafa
amekataa kumpa mwanawe wa kiume bangi kama matibabu
inavyotakikana-kupitia moshi na mvuke. Mtoto huyo anapasawa kutumia
Bangi kama dawa kupambana na ugonjwa wake wa Kifafa kwa maagizo ya
daktari.
Liam McKnight mwenye umri wa miaka sita napenda kucheza
na ndiye wa kwanza kila mara kukimbia kuelekea mlangoni.Mamake
mzazi,Mandy,anasema kuwa mwanawe anapenda kujua nani anawatembelea.
Familia
hiyo ya McKnight inayoishi jijini Otawa nchini Canada ina wageni wengi
wanaowatembelea-kutoka kwa wanachama wa kukindi cha densi anachoshiriki
binti yao,na hata wauguzi wa kutamka,wa kunyosha viungo vya
mwili,wataalam wa kusikiza-wote wanaomtembelea Liam.
Liam ana
ugonjwa unaojulikana kama Dravet ambayo,ni aina kali sana ya kifafa.Afya
yake hudhoofika mara kwa mara lakini baada ya kufanyiwa majaribio kadha
wa kdha ya matibabu ya ugonjwa huo, anglau hali yake imeimarika kidogo.
Mamake Liam humpa mafuta ya Bangi, ambayo yemtolewa kwa sehemu changa sana ya mmea huo. Mwezi
Juni mwaka huu,siku kabla Liam kuanza kutumia mafuta hjayo ya
Bangi,(iliyotengezwa kutoka kwa aina ya bangi yenye ufanisi) alizirai
kama mara 67. Katika siku kumi zilizofuatia alizirai tu mara moja. Nchi nyingi duniani zinakabiliwa na changamoto za kuidhinisha matumizi ya Bangi.
Tatizo ni kuwa matibabu ya Liam
ni haramu. Kutumia dawa inayotengezwa kwa Bangi inakubalika Canada
lakini lazima iwe tu majani ya Bnagi yaliyokaushwa au mvuke wa majani
hayo.
Kwa Mandy hilo haliwezakni kwa mwanawe kuvuta moshi wa Bangi akiwa umri huo mdogo.
Matoto mdogo anawezaje kuvuta Bangi? anauliza mamake Liam.
Mapema
mwaka 2001, Canada iliruhusu wagonjwa wanaohisi uchungu mwingi kutumia
Bangi kama matibabu. Lakini hakuna majaribio yaliyofanyiwa mafuta ya
Bangi kujua usalama wake kwa afya ya mtu.
Liam ana umri mdogo sana
lakini anaweza kutumia mvuke wa Bangi lakini mamake Liam anasema vipimo
vinyovyofa akwa afya ya Liam ni vya mafuta ya Bnagi.
Mamake Liam
aliwahi kuiandikia serikali Barua kuielezea kuhusu masaibu yake
kuhusiana na matibabu ya Liam. Lakini waziri wa afya alimjibu kwa kusema
anaelewa masaibu ya mtoto Liam wakati akikabiliana na ugonjwa wake
hatari wa kifafa. Lakini alisisitiza kuwa hadi leo serikali bado
haijaidhinisha matumizi ya mafuta ya Bangi wala uuzaji wa mafuta hayo
nchini Canada.
Matumizi ya mafuta ya Bangi, yaliruhusiwa mjini
Minnesota Marekanimwezi Mei, lakini sheria hiyo haitaanza kutumika hadi
Julai mwaka 2015.
Sheria za Bangi kote duniani zinatofautiana.
Mamake
Liam anafahamu kuwa anavunja sheria pamoja na kufahamu athari z
akutumia mafuta ya Bangi. ''Je nahofia kuwa navunja sheria? ndio. Lakini
nahofia zaidi ikiwa hatutafanya chochote hali ya afuya ya mtoto wangu
itazorota.
Kwetu Mafuta ya Bangi ndio tiba anayohitaji mwanangu.
Hatukuwa na mda wa kusubiri majaribio kufanywa. Kwa kila siku, Liam hula
kijiko kimoja cha Bangi ikiwa imechanganywa na mafuta ya nazi.
Mzunguko wa 14 umekamilika kwa timu zote 20 za ligi kuu ya England kushuka viwanjani.
Chelsea,
wameendeleza wimbi la ushindi na kukataa katakata kuzipa nafasi timu
nyingine 19 kupunguza pengo la pointi lililopo kati yake na timu hizo.
Sergio Aguero, mchezaji wa Manchester City akishangilia moja ya magoli yake katika ligi kuu ya EnglandChelsea imeendelea kuwa na
tofauti ya pointi sita na Man City inayoifuatia baada ya kuirarua
Tottenham mabao 3-0, huku Manchester City yenye pointi 30 ikiisasambua
Sunderland magoli 4-1. Sergio Aguero ameifungia timu yake ya Manchester
City magoli mawili katika mchezo huo, huku Jovetic na Zabaleta kila
mmoja akifunga bao moja. Magoli ya Chelsea yamefungwa na Hazard, Drogba na Remy. Wachezaji wa Arsenal Santi Carzola akishangilia goli na Alexis Sanchez
Mchezo mwingine wa Jumatano
usiku, ulikuwa kati ya Arsenal na Southampton wanaoshikilia nafasi ya
tatu katika msimamo wa ligi kuu ya England. Mchezaji Alexis Sanchez
ndiye aliyekuwa shujaa na kuwanyanyua vichwa mashabiki wa Arsenal pale
alipoifungia timu yake goli pekee katika mchezo huo ikiwa ni dakika ya
89 ya mchezo, uliofanyika uwanja wa Emirates na hivyo kujikusanyia
pointi tatu muhimu kuelekea kileleni.Arsenal inashikilia nafasi ya sita
ikiwa na pointi 23, pointi 13 nyuma ya vinara Chelsea yenye pointi 36.
Everton na Hull City ziligawa pointi baada ya kufungana bao 1-1.
Hadi
kufikia mzunguko huo wa 14, Chelsea inaongoza kwa kujikusanyia pointi
36, ikifuatiwa na Man City yenye pointi 30, Southampton ni ya tatu na
pointi 26, Huku Manchester United kiwa nafasi ya nne na pointi 25 na
nafasi ya tano inashikiliwa na West Ham yenye pointi 24.Ivabaada
Upangaji wa makundi ya timu kumi na
sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu wa
Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17, 2015.
Upangaji
wa makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial
Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae
mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo baada ya kutaka
mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao
umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu
nyingi zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni
moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani,
pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015: Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
Wenyeji
Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano
hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu
zilizopangwa kundi hilo.
Misri imefunga lango la mpaka wa Rafah unaounganisha nchi hiyo na Gaza Katika maelezo yaliyoandikwa na Kamati Kuu ya Mipaka na Milango ya mpakani, inayohusishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya Palestina iliyoko Gaza, iliarifiwa kwamba serikali ya Misri ilifunga lango la mpaka wa Rafah hadi amri ya pili itakapotolewa baada ya Wapalestina 554 waliokwama nchini humo kuvuka Gaza.
Viongozi wa Misri waliwahi kufungua lango la mpaka wa Rafah pia siku ya jumatano iliyopita kwa ajili ya Wapalestina waliokuwa wakisubiria kupita Gaza.
Kutokana na vizuizi vya Israel, ‘’Lango la Pekee la Gaza kwa dunia’’ la Rafah limekuwa likifungwa mara kwa mara baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotekelezwa mwezi Julai 2013 nchini Misri. Hatimaye mnamo tarehe 24 Oktoba, baada ya mashambulizi kutekelezwa katika vituo 2 vya usalama mkoani Sinai Kaskazini, serikali ya Misri ilitoa ilani ya dharura ya miezi 3 kwenye eneo hilo kwa madai ya ‘’kutatua mizizi ya tatizo la ugaidi’’, na kuchukua hatua ya kufunga lango la mpaka wa Rafah katika mchakato huo.