Mchana wa jana basi ya RUWINZO DAR kwenda SONGEA na Basi la IFAKARA EXPRESS
yamegongana maeneo ya mikumi. Inasemekana Abiria 7 wamefarik hapo hapo.
Tuendelee kuombea Taifa letu .
Mwandishi wetu alifanikiwa kuongea na mmoja wa mhanga wa ajali hiyo alisema "Hali halisi
ya ajali ni kuwa na mwendo wa kasi dereva wetu tulipofika mikumi majira
ya saa 5:30 asubuhi tukitokea dar es salaam kuelekea malininyi-mahenge
Gari nililolipanda mimi linaitwa MSANGA line express ambalo linafanya
safari zake Dar,ifakara-malinyi tulipofika
mikumi mbele yetu kulikuwa na lori lenye namba za usajili T 299 nalo lilikuwa linatoka
dar-iringa dereva wetu alikuwa ana-over take hilo lori kabla hajamaliza
kupita hilo lori alikutana uso kwa uso na basi la ruwenzo ambalo lilikuwa
linatoka njombe kuelekea dar sasa dereva wetu akaona amkwepe huyu
mwenye basi la ruwenzo anafanya hivyo na ruwenzoakawa ameshaingia kwahiyo amelipiga
kwa nyuma Gari letu na hapo hapo Gari letu kwa sababu lilikuwa na mwendo
kasi lilivyopigwa likabilingika Mara moja juu chini alafu likakaa sawa
na kuziba njia marehemu nilioshuhudia kwa macho yangu ni 7 majeruhi
usiseme wengine wamekatika miguu wangine mikono wangine kichwa vinavuja
damu kama maji sasa nilivyokuwa nahojiwa na Mkuu wa polic wa wilaya
akapigiwa simu tena kusema waliobebwa Hosp.wamefaliki 3 so ukijumlisha
utapata 10 ili kuna uwezekano wa waliofariki wakaongezeka maana hali zao ni mbaya sana
No comments:
Post a Comment