Wednesday 11 March 2015

Mlinzi wa Dk. Silaa aendelea kusota rumande

Image result for Mlinzi wa silaaKHALID Kangezi, mlinzi binafsi (PSU) wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi kuhusu tuhuma dhidi yake.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Kinondoni, Camillus Wambura alisema uchunguzi unaendelea dhidi ya Kagenzi ambaye alifikishwa katika Kituo cha Polisi Osterbay juzi.
“Suala hili nilitakiwa kulitolea taarifa kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, lakini sikumpelekea kwa sababu uchunguzi haujakamilika.
“Bado tunaendelea kumchunguza mtuhumiwa, zipo taarifa mbalimbali ambazo hazijakamilika zitakapokamilika tutampelekea Kamishna Kova aweze kulizungumzia suala hilo.
“Tunaomba muwe na subira tuone itakuwaje na nitawasisitiza wapelelezi waongeze kasi ya uchunguzi tuweze kupeleka taarifa kwa Kamishna aweze kulitolea ufafanuzi katika jamii,” alisema Wambura.
Kangezi ambaye amekuwa mlinzi wa Dk. Slaa kwa miaka miwili, inadaiwa alikuwa akitumiwa na vyombo vya Usalama wa Taifa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuvujisha siri za chama hicho ikiwamo kupewa kazi ya kumuua Katibu Mkuu huyo wa Chadema.
Hata hivyo, jana wanasheria wa Chadema waliitwa Kituo cha Polisi Osterbay kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo.

No comments: