Rais Obama amemtumia salaam za
pongezi waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kutokana na ushindi
uliokipata chama chake katika uchaguzi uliofanyika Jumanne.
Lakini
Bwana Obama ameelezea dhamira yake ya kuupatia ufumbuzi mgogoro kati ya
Israel na Wapalestina kuwa ni kuunda taifa la Palestina.Awali Ikulu ya Marekani ilielezea wasiwasi kuhusu ahadi ya Bwana Netanyahu wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba asingeruhusu kuundwa kwa taifa la Palestina.
Waziri mkuu wa Israel tangu wakati huo amelegeza msimamo wake, akisema atakubali suluhisho la kuwepo mataifa mawili jirani endapo usalama katika eneo la Mashariki ya Kati utaimarishwa.
No comments:
Post a Comment