Afisa mmoja wa polisi amekamakwa na pembe ya faru ilio na thamani ya dola 40,000.
Tayari amefikishwa mahakamani.Afisa huyo na wenzake watatu walipatikana wakiwa katika harakati ya kuuza pembe hizo kwa wapelelezi wa shirika la wanyama pori nchini Kenya KWS.
Mshukiwa huyo ni afisa wa cheo cha chini katika kikosi cha polisi cha Kenya .
Aliingizwa mtengoni na maafisa wa shirika la wanayama pori waliojifanya kuwa wanunuzi wa pembe hiyo ya faru.
Wakati maajenti hao walipojaribu kumkamata afisa huyo alionya kuwapiga risasi lakini akashindwa nguvu.
Alipelekwa katika kizuizi usiku wa jumatatu pamoja na washukiwa wengine.
Mshukiwa wa nne alitoroka.
Pembe za faru hudaiwa kuwa na thamani zaidi ya dhahabu barani Asia,ambapo pembe zinazoibwa barani Afrika hupelekwa.
No comments:
Post a Comment