Klabu tatu za Ligi Kuu ya China zimeripotiwa kuitamani saini ya beki wa Juventus Dani Alves.
Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur Andre Villas-Boas
ambaye kwa sasa anainoa Shanghai SIPG anaongoza katika kinyang’anyiro cha
kuwania saini ya nyota huyo wa anayekipiga Serie A.
France Football kimeripoti kuwa Villas-Boas wa SIPG yupo
tayari kumlipa Mbrazili huyo kitita cha paundi 165,000 kwa wiki kumtoa Serie A
kutua kwenye ligi hiyo ya matajiri wa Mashariki ya Mbali.
Alves alitua Turin majira ya joto baada ya kuitumikia
Barcelona kwa kipindi cha miaka nane, lakini ametokea kuzivutia klabu za Asia.
Kwa mujibu wa francefootball.fr, Hebei China Fortune,
Tianjin Quanjin na Shanghai SIPG zote zinamtaka mkongwe huyo wa miaka 33 kwenye
kikosi chao.
Bado haijadhihiri wapi Alves atapachagua kuwa mustakabali
wake, lakini beki huyo wa Kibrazili amebakiwa na miezi sita tu kwenye mkataba
wake na miamba hao wa Italia.
Alves amefunga mara mbili katika mechi 13 za
michuano yote msimu huu
No comments:
Post a Comment