Polisi wilayani Igunga mkoni Tabora wamewakamata watu
watatu wakiwa na noti bandia za shilingi 10,000 zipatazo mia nane sawa
na shilingi milioni nane wakiwa wamezihifadhi kwenye buti ya gari yao
ndogo
Watuhumiwa waliokamatwa na noti hizo ni Luneka Magasha 35)
mkazi wa Igunga, Zengo Magasha (25) mkazi wa mkoa wa Lindi na James
Hangalu mkazi wa Dar es salaam
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Hamisi Selemani
alithibitisha kukamatwa kwa watu hao na kusema kuwa polisi walipata
taarifa ya kuwepo kwa watu wenye noti za bandia na baada ya taarifa hiyo
walikwenda eneo la tukio na kuwakuta watu hao waikiwa na gari ndogo
yenye namba za usajili T 964 BEC
Aidha kamanda Selemani alisema kuwa baada ya kuwapakua
kwenye gari yao walikuta shilingi million nane na elfu kumi kwenye buti
ya gari hiyo
“Baada ya kuwahoji watu hao walikiri kuwa noti hizo ni
zabandia na nimali yao na walikuwa wamejipanga kuzisambaza katika minada
ya ng’ombe ya Igunga na Ibologelo” alisema kamanda selemani
Kamanda aliongeza kuwa fedha hizo pamoja na gari waliokutwa
nayo vinashikiliwa na jeshi la polisi, na ametoa wito kwa wananchi kuwa
makini katika biashara zao na kwenye magulio mbalimbali mkoani humo.
No comments:
Post a Comment