Tuesday, 17 January 2017

Mtoto aliyezikwa afufukaMBEYA: Mtoto aliyezikwa jana akutwa chumbani kwake mara baada ya mazishi
Wakazi wa eneo la Isanga katika jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa na mikasa, ushilawadu na matukio ya vioja, baada ya mtoto wa miaka 9 aliyekuwa amezikwa jana kwenye makaburi ya Isanga kukutwa akiwa kitandani kwake amelala usingizi mara baada ya kurejea kutoka makaburini.
Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao amelala kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhi hii kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea  .

No comments: