Washtakiwa wanne katika shauri la kufanya vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa la kimtandao wameachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kutupilia mbali hoja za kuzuia dhamana zao zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi,
Wilbert Chuma leo Desemba 15, baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa
utetezi, Mashaka Tuguta, Ogastini Kulwa na Jebra Kambole kuwa hoja
zilizowasilishwa na upande wa mashtaka ni dhaifu mbele ya macho ya sheria.
Washtakiwa katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe
Suleiman na Janeth Shonza wanaodaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote
kuwa wanawake.






