SERIKALI imesema kama Shirika la Afya Duniani (WHO),
litapitisha matumizi ya dawa mpya ya ugonjwa Ukimwi wataitumia, lakini
kwa sasa haiwezi kuzungumzia tafiti za ugonjwa huo ambazo zipo nyingi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John, amesema kwa sasa zipo tafiti
nyingi, lakini wao kama wizara wanasubiri mwongozo kutoka WHO ambao
ndiyo unathibitisha ubora wa dawa na matumizi yake.
“Zipo tafiti nyingi tunazisikia zinafanyika, lakini hili la
Ukimwi ni mapema mno kulizungumzia ila kinachohitajika ni kusubiri
mwongozo wa WHO ambao ndio wanatuongoza kwenye orodha ya dawa na
matumizi yake katika magonjwa mbalimbali,” alisema John.