Richie ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Weekend
Breakfast siku ya jumapili,, na kusema kuwa baada ya filamu yake kuingia
kwenye hizo category mbili aliamini yeye anaweza hivyo alitaka ashinde
zote mbili, ingawa kwenye tuzo za Tanzania haikuwahi kuwa nominated.
“Ningechukua zote mbili, nilipochukua ile moja nilikasirika, naamini
kama ninajua, tuzo za Tanzania haikupita hata kuwa nominated, nilikwenda
Nigeria nikiwa na uhakika ninaenda kushinda”, alisema Richie.
Pamoja na hayo Richie amesema sio mtu wa majivuno na kujionyesha kama
ilivyo kwa wengine, kwani tuzo hiyo sio ya kwanza kuchukua, kwani
alishawahi kuchukua tuzo kubwa zaidi ya hiyo mwaka 2001, pamoja na
uvumilivu na bidii ndio umemfikisha hapo.