mwenyekiti wa tume ya uchaguzi mkuu nchini Gambia imemtangaza aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchinu humo Adama Barrow kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu kwa kumshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kwa idadi ya kura 263,515 dhidi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh akipata kura 212,099.
Kutokana na ushindi huo Barrow ameumaliza utawala wa Yahya aliyetawala kwa miaka 22 baada ya kuchukua nchi kwa njia ya mapinduzi.
Adama alipokuwa akihojiwa amedai kuwa anachokisubiria ni simu kutoka kwa Yahya kukubali matokeo pia ameongeza kwa kusema anawashukuru wananchi wa Gambia kwa kumpa kibali cha kuwaongoza anaahidi kuwatumikia ipasavyo kwa kuilinda na kuitetea katiba
No comments:
Post a Comment