Washika bunduki wa London, Arsenal
wamekaa kileleni mwa ligi ya England kwa pointi 39 baada ya kuichapa
Bournemouth kwa mabao 2-0.
Arsenal walipata mabao yao kupita kwa
beki Gabriel Paulista aliyefunga bao la kwanza Dakika ya 27 ya mchezo
kisha kiungo wa Kijeruman Mesut Ozil, akahitimisha kazi kwa bao la pili
alilolifunga katika dakika ya 63.
Maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini walifanya maandamano hapo jana katika miji mikubwa ya Afrika Kusini kwa ajili ya kumpinga rais Jacob Zuma.
Waandamanaji hao waliokusanyika katika mitaa ya miji ya Johannesburg, Pretoria, Cape Town na Port Elizabeth, walimshutumu Zuma kwa madai ya ufisadi na kuzorotesha uchumi wa nchi.
Maandamano hayo yaliongozwa na kiongozi wa zamani wa muungano wa biashara Zwelinzima Vavi aliyemlaumu Zuma kwa kumbadilisha waziri wa fedha mara mbili ndani ya wiki moja.
Mnamo tareheh 9 Desemba, Zuma alimfuta kazi aliyekuwa waziri wa fedha Nhlanhla Nene na kumteua David van Rooyen kuziba pengo hilo.
Ndani ya wiki hiyo, Zuma baadaye akamuondoa David van Rooyen na kumteua Pravin Gordhan kuwa waziri mpya wa fedha.