Tuesday, 18 August 2015

Wanachama wa CCM waandamana kibondo kupinga uteuzi wa mgombea ubunge

Mamia ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM katika wilaya ya Kibondo wameanadamana na kuvamia ofisi za chama hicho wakipinga mgombea aliyeshinda katika kura za maoni Jamal Abdalah kutoteuliwa na halmashauri kuu ya taifa ya CCM kuwania ubunge katika jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo.

Wanachama wa CCM waandamana kibondo kupinga uteuzi wa mgombea ubunge

Mamia ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM katika wilaya ya Kibondo wameanadamana na kuvamia ofisi za chama hicho wakipinga mgombea aliyeshinda katika kura za maoni Jamal Abdalah kutoteuliwa na halmashauri kuu ya taifa ya CCM kuwania ubunge katika jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo.

Wanachama wa CCM waandamana kibondo kupinga uteuzi wa mgombea ubunge

Mamia ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM katika wilaya ya Kibondo wameanadamana na kuvamia ofisi za chama hicho wakipinga mgombea aliyeshinda katika kura za maoni Jamal Abdalah kutoteuliwa na halmashauri kuu ya taifa ya CCM kuwania ubunge katika jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo.

Viongozi wa UKAWA wakamilisha ziara ya kutafuta wadhamini visiwani Zanzibar.

Mgombea urais wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch (UKAWA) Mh Edward Lowassa amekamilisha ziara ya kutafuta wadhamini katika visiwa vya Zanzibar na amewaahidi wananchi wa visiwa hivyo kutumia uwezo wake wote kushughulikia kero za muda mrefu zinazowakabili ikiwemo ya muungano ukiukwaji wa haki na wizi wa kura unaofanyika wakati wa uchaguzi.
Akizungumza na wananchi hao katika viwanja vya Kibanda Maiti visiwani Zanzibar Mh Lowassa amesema hatua iliyofikia sasa suala la kuiondoa CCM madarakani halina mjadala kilichobaki ni utekelezaji ambao asilimia kubwa uko mikononi mwa wananchi.

Sunday, 16 August 2015

Askofu Shoo awa mkuu mpya KKKT

Askofu Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la
Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Frederick O. Shoo (kulia) akiwa na Askofu anayemaliza muda wake, Dk Alex Malasusa baada kuchaguliwa juzi usiku kwenye mkutano ulifanyika Arusha

 Dk Shoo, ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, alichaguliwa juzi usiku katika siku ya tatu na ya mwisho ya mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini (Tuma) jijini Arusha baada ya kuwashinda maaskofu wenzake wawili, katika uchaguzi uliokuwa na kila aina ya ushindani

Askofu Askofu Dk Fredrick Shoo amechaguliwa kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), akichukua nafasi ya Dk Alex Malasusa aliyemaliza kipindi chake cha miaka minane.
Dk Shoo, ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, alichaguliwa juzi usiku katika siku ya tatu na ya mwisho ya mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini (Tuma) jijini Arusha baada ya kuwashinda maaskofu wenzake wawili, katika uchaguzi uliokuwa na kila aina ya ushindani.
Waliokuwa wakichuana kuwania nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na Halmashauri Kuu ya KKKT ni Askofu Dk Stephen Munga wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Askofu Charles Mjema wa Dayosisi ya Pare na Dk Shoo.
Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Dk Malasusa, ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, alimtangaza Dk Shoo kuwa mkuu wa kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne baada ya kupata kura 153, huku Dk Munga akipata kura 67, ikiwa ni baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara tatu kutokana na mshindi kutopata zaidi ya theluthi mbili ya kura zote.

Msafara wa Lowasa wapigwa mabomu jana jijini Arusha

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa akizungumza na polisi kwenye Daraja la Nduruma mjini Arusha, baada ya kufunga Barabara ya Sabasaba wakati akitokea kwenye Uwanja wa Tindigani. Polisi walimkubalia kupita barabara hiyo na kuzuia msafara wake
 
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa jana kwa mara ya kwanza alikumbana na joto la upinzani baada ya msafara wake kushambuliwa na mabomu ya polisi.
Tukio hilo, ambalo lilifanyika mbele ya msafara wa Lowassa, lilitokea jana eneo la Daraja la Nduruma katika Jiji la Arusha na kusababisha umati wa watu kutawanyika na wengine kutelekeza magari yao.
Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkaribisha kwenye chama hicho wakati wa mkutano mkuu alimwambia; “Mzee huku inabidi uwe unafanya mazoezi kidogo, kuna mabomu huku.”
Lowassa alikumbwa na kadhia hiyo, akiwa njiani na mgombea mwenza, Juma Duni Haji na viongozi wengine wa Ukawa, wakitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), huku wakiwa wamesindikizwa na umati wa watu na magari.

Maeflu wajitokeza Kumlaki Lowasa Arusha

Maelfu ya wananchi wa ndani na nje ya mkoa wa Arusha wamejitokeza kumpokea na kumsikiliza mgombea urais wa CHADEMA kupitia UKAWA na waziri mkuu wa zamani Mh.  Edward Lowasa huku wakishuhudu wanachama wa (CCM) na viongozi akiwemo aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani Mh.Laurence Masha.
Wengine waliojiunga na CHADEMA ni pamoja na katibu wa CCM wa wilaya ya babati  Bw,Daniel Porokwa,Mwenyekiti wa UWT,wa wilaya ya karatu  bi fabiola  manimo  katibu wa UWT wa wilaya ya Siha,na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa  Arusha kwa zaidi ya miaka 20 Mh.Yona Nnko.

Saturday, 15 August 2015

Lema na Mbatia watoa onyo Kali kwa Jeshi la Polisi


Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Godbles Lema amelilaumu jeshi la polisi Mkoani arusha kwa kujaribu kumzuia  msafara wa aliyekuwa waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya Nne  na Mtia nia wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Chadema na UKAWA  kuwasili katika viwanja vya mkutano wa kumtambulisha Mh. Edward Lowasa kwa wananchi wa Arusha kama mgombea ambaye atapeperusha bendera ya chadema na Ukawa
Polisi waliwazuia wanachama wa Chadema na Ukawa ambao waliandamana na msafara wa Mh. Lowasa kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mkoan Kilamanjaro KIA, walipofika maeneo ya jimbo la Arumeru mashariki mji mdogo wa USA River karibu na Mto nduruma walikuta jeshi la polisi wakiwa wameweka vizuizi na kuanza kurusha mabomu ya machozi kuwatawanyisha wanachama wa Ukawa walioandamana na Lowasa.
Lema aliendelea kusema  “serikali na jeshi la polisi wanajaribu kuwaogopesha wananchi ili ccm waweze kuiba kura uchaguzi ujao “ Pia atoa salamu kwa IGP wa Arusha  “ Kama amewafundisha wanajeshi wake kuuwa basi yeye kajifunza kutembea akiwa maiti “
Lema akizungumzia swala la Jeshi la Polisi la Mkoa wa Kilimanjaro kumzuia Lowasa kwenda kumzika aliyekuwa mwanachama wa chama cha Mapinduzi  Mzee Kisumo  Alisema  haoni sababu ya maana ya lowasa kuzuiliwa kwenda msibani kwani haijawahi tokea duniani mtu akazuiliwa kwenda msibani  bali anahisi ni woga wa Rais Jakaya Kikwete kuwa atafunikwa na Lowasa katika msiba huo.
Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia nae awaonya jeshi la polisi kwa kuwaasa mkuu wa jeshi la Tanzania Mangu kuwa kama wataendelea kuwaonea wananchi kwa kuwapiga mabomu ovyo ovyo basi wasubirie mahakama ya ICC kuwatia mbaroni
Licha ya kuwaasa wakuu wa jeshi la polisi amemwaga sifa kwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kwa kusimamia Mkutano wao kwa makini na bila Uonevu wa aina yoyote  

Viongozi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro wajiunga Chadema.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) na katibu wa fedha na uchumi wa chama cha mapinduzi(CCM) wa mkoa wa Kilimanjaro wamejiuzulu uongozi wa chama hicho na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo( Chadema).
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini moshi viongozi hao ambao ni mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM)mkoa wa Kilimanjaro Bw.Fredrick Mushi na katibu wa fedha na uchumi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Paul Matemu wamesema wamechoshwa na mwendo wa chama hicho.

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa vibaya katika ajali mkoani Geita.

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha gari mbili za mizigo na basi la abiria mali ya kampuni ya Sabuni Express katika kijiji cha Lubambangwe wilaya ya Chato mkoani Geita wakati dereva wa basi akijaribu kukwepa kugongana uso kwa uso na gari la mizigo hali iliyomsababisha kupalamia gari bovu lililoengeshwa barabarani ili kunusuru maisha ya watu.

NEMC imekifunga kiwanda cha kusindika nyama ya Punda mkoani Dodoma.

Baraza la taifa la usimamizi wa mazingira {NEMC} limekifungia kiwanda cha Huwa Cheng Company Limited kilichopo mjini Dodoma na kukitoza faini ya shilingi milioni 200 baada ya kubaini kiwanda hicho kinajihusisha na usindikaji wa nyama ya Punda kinyume na utamaduni wa watanzania huku mazingira yake yakiwa hatarishi kutokana na uchafu unaozalishwa kuzagaa kwenye makazi ya watu.
Ni mabishano makali baina ya wamiliki wa kiwanda hiki raia wa uchina na maofisa wa NEMC yaliyochukua muda mrefu kabla ya maofisa hao kutoa tamko la kufungwa kwa kiwanda hicho ambacho mbali na kuzalisha nyama ya Punda ambayo ni kinyume na utamaduni wa watanzania lakini pia mazingira ya uzalishaji wake ni hatarishi kwa afya za wafanyakazi na majirani wa eneo hilo.

Friday, 14 August 2015

Mh.Lowassa ashindwa kwenda kumzika Kisumo, msafara wake wazuiliwa na polisi.

Waziri mkuu wa zamani Mh Edward Lowassa ameshindwa kuhudhuria mazishi ya mwanasiasa mkongwe hayati mzee Peter Kisumo yaliyokuwa yanafanyika Usangi mkoani Kilimanjaro baada ya msafara wake kuzuiliwa na polisi katika wilaya ya Mwanga kutokana na kuongozana na wananchi wakiwemo vijana waliokuwa na pikipiki waliokuwa wanakwenda kwenye mazishi.
Gari la Mh Lowassa ambaye pia ni mgombea urais wa Chadema akiwakilisha Ukawa lilianza kufuatwa na magari mengine ya watu binafsi na pikipiki baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akitokea na Dar es Salaam na alipofika Moshi kundi la vijana walifunga barabara na kulazimika kuingia katika hotel ya kizi ambako pia walimfuata na kuzingira lango kuu na licha ya kuwasihi kuwa wampe nafasi aende kwenye mazishi vijana hao waliendelea kulifuata gara lake. 

Mtoto apata Mtoto huko Paraguay

Kampeni imeanzishwa kupinga ubakaji kwasababu ya kisa cha binti huyo.
Binti wa miaka kumi na mmoja nchini Paraguay aliyedai kubakwa na baba yake wa kambo amejifungua mtoto wa kike baada ya mamlaka nchini humo kumzuia asitoe ujauzito aliokua nao.
Madaktari katika mji mkuu wa Asuncion wamesema binti huyo na mtoto wake aliyejifungua kwa njia ya upasuaji wanaendelea vizuri.

Fidel Castro aandika barua ya wazi Cuba

Rais wa zamani wa Cuba,Fidel Castro
Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro ametimiza umri wa miaka 89 kwa kuandika barua ya wazi kwa taifa lake.
Barua hiyo ilichapishwa katika gazeti la serikali la Granma ambapo hajazungumzia lolote kuhusu ufunguzi wa ubalozi mpya wa Marekani jijini Havana utakavyofanya kazi na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.

Thursday, 13 August 2015

Ban Ki-Moon amtimua kazi Babacar Gaye

Babacar Gaye
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, amesema amemfukuza mkuu wa kulinda amani toka UN nchini Afrika ya kati baada ya kutuhumiwa kuhusika na madai ya unyanyasaji wa watoto kingono.
Bwana Ban amesema mwanadiplomasia wa Senegal Babacar Gaye angeachia ngazi kama mkuu wa ujumbe. Ban aliongeza kuwa alipatwa na hasira na aibu baada ya taarifa hizo za unyanyasaji wa ngono na ukandamizaji kwa watoto.

Wednesday, 12 August 2015

Shambulio la bomu latekelezwa kaskazini mashariki mwa Nigeria

Shambulio la bomu NigeriaShambulio la bomu latekelezwa kaskazini mashariki mwa Nigeria

Watu 47 wameripotiwa kufariki kati shambulio la bomu lililotekelezwa katika jimbo la Borno Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria.
Shambulio hilo limetekelezwa katika soko ambalo linapatika katika jimbo hilo.

Vifungu vyote vya sheria ya mtandao vilivyolalamikiwa na wadau vimerekebishwa.

Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Dk Ally Simba amesema vifungu vyote vilivyolalamikiwa na wadau kuhusu sheria ya makosa ya mtandao vimefanyiwa marekebisho huku akiwataka wananchi hasa watumiaji wa mitandao kujiandaa kuipokea sheria hiyo.
Rai hiyo imekuja zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Septemba mosi mwaka huu ambapo amesema kuanza kwa sheria hiyo kutasaidia mambo mengi sana ikiwemo kulinda mifumo ya msingi ya tehama na kutolea mfano wa mitandao ya simu za mkononi.
 

Mwenyekiti wa CCM wilayani Sumbawanga Bw Emmanuel Kilindu ajiuzulu.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa wilaya ya Sumbawanga mjini Bw Emmanuel Selemani Kilindu, amechukua hatua ya kujiuzulu wadhifa wake huo kufuatia kuhitilafiana kwa kiwango kikubwa na mbunge anayemaliza muhula wake, na kudai kuwa licha ya kukabiliana na changamoto nyingi za kiutendaji lakini pia anayaweka maisha yake kwenye hatari kubwa.

Tuesday, 11 August 2015

Chelsea kukata rufaa dhid ya kadi nyekundu ya Thibaut Cortois

Thibaut Courtois
Klabu ya Chelsea inatarajiwa kukata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa mlinda mlango Thibaut Courtois katika mchezo uliopigwa jumamosi dhidi ya Swansea ambao uliisha kwa droo ya magoli mawili katika uwanj wao wa nyumbani Stamford Bridge.

Yaya Toure aiua West Brom

Yaya Toure akiinua mkono kufurahia ushindi

Yaya Toure aliiongoza Man City katika ushindi mnono dhidi ya West Brom ambapo Raheem Sterling aliyesajiliwa majira ya joto kwa dau la pauni milioni 49 akicheza mchezo wake wa kwanza kwa timu yake mpya.

Monday, 10 August 2015

Zaidi ya wanachama 100 wa CCM warejesha kadi na kujiunga na Chadema Bukoba.

Zaidi ya wanachama miamoja akiwemo mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Bukoba jimbo la Bukoba mjini ambae pia ni diwani wa kata ya kahororo Chief Kalumuna wamerejesha kadi za chama cha mapinduzi na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei amesema wanachama hao ambao wengiwao wamepelekea kadi hizo kimyakimya kwa muda wa siku saba na kufikia wanachama miamoja hamsini wameamua kufanya hivyo kwaajili ya kumuunga mkono waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa na kuhakikisha anapata kiti

Watanzania watakiwa kuchambua na kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.

Watanzania wametakiwa kuwachagua viongozi walio na moyo wa dhati wa kuwaletea maendeleo ya haraka kwa kutumia rasilimali za nchi zilizopo na kuachana na viongozi wanaotumia mbwembwe nyingi kujitangaza kwa kuwa nchi haihitaji viongozi wa mbwembwe bali wenye maamuzi kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa kuwa viongozi wenye ndimi mbili na mbwembwe za nguvu ya fedha hawafai kuwaongoza na kuwaondoa katika umasikini watanzania.

Kimbisa akanusha kuhama ccm

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe
MWENYEKITI wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amekanusha uvumi kuwa ameungana na wenyeviti wengine wa mikoa wa CCM kukihama chama tawala nchini. Amesema wanaomzushia washindwe na walegee, kwani moyo na mwili wake upo CCM na kwamba kamwe hawezi kuhama.
Aliyasema hayo jana mjini hapa kutokana na kuwapo kwa taarifa amekihama chama hicho. Awali, jana kulikuwa na taarifa za Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo ole Nangole kuhamia Chadema, kama ilivyokuwa kwa Mgana Msindai, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida aliyetangulia Chadema wiki iliyopita baada ya kushindwa kura za maoni ndani ya CCM.

Katibu mwenezi wa Chadema achukua fomu kugombea ubunge kupitia ACT-wazalendo.

Aliyelkuwa katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika wilayaya Butiama Bw Richard Choge Magori amekihama chama hicho kisha  kuijunga na chama cha ACT wazalendo kabla ya  kuteuliwa kwa ajili ya kugombea ubunge katika jimbo jipya la Butiama mkoani Mara.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu na mkurugenzi wa wilaya ya Butiama kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi ili kumwezesha kugombea ubunge katika jimbo hilo, kada huyo mpya wa chama cha ACT- wazalendo, amesema kuwa ameamua kujiunga na chama hicho na kugombea ubunge katika jimbo hilo baada ya kubaini wanachama

Sunday, 9 August 2015

Lowasa kuchukua fomu ya urais NEC kesho

MGOMBEA urais wa vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kesho atachukua fomu ya uteuzi wa urais katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Akizungumzia katika Makao Makuu ya chama cha NCCR-Mageuzi Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, alisema msafara wa kumsindikiza Lowassa, utaanzia Makao Makuu ya CUF, Buguruni asubuhi saa tatu kwenda NEC ambapo saa tano asubuhi mgombea huyo atachukua fomu.

Israel yawakamata 7 waliochoma Wapalestina

Israel yawakamata 7 waliochoma Wapalestina
Maafisa wa Polisi nchini Israeli wamesema kuwa wamewakamata watu 7 wanaoshukiwa kwa kuvamia nyumba moja ya mpalestina katika ukingo wa magharibi na kuiteketeza moto.
Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi uliopita lilisababisha kifo cha mtoto wa mwaka mmoja u nusu.
Shambulizi hilo lililotekelezwa na walowezi wa Kiyahudi lilimuacha bwana Dawabsheh mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakiuguza majereha mabaya.

Gari lenye uwezo wa kupita juu ya milima na majabali

Gari lenye uwezo wa kupita juu ya milima na majabaliGari lenye muundo wa pikipiki linastaajabisha kwa kuwa na uwezo wa kupita katika ardhi zenye mawe makubwa na milima mirefu bila ya kukumbwa na matatizo ya kiufundi.

Bofya hapa kuona video ya gari hilo

Rais Buhari atoa agizo la uundaji wa silaha kwa Wizara ya Ulinzi nchini Nigeria

Nigeria kuanza kuunda silaha ndani ya nchiRais Buhari atoa agizo la uundaji wa silaha kwa Wizara ya Ulinzi nchini Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammed Buhari, ametoa agizo la kuanzishwa kwa shughuli ya uundaji wa silaha kwa Wizara ya Ulinzi nchini ili kusaidia mapambano dhidi ya kundi la Boko Haram.
Akitoa hotuba yake kwenye hafla ya chuo cha kijeshi iliyoandaliwa katika mji mkuu wa Abuja, Buhari alisema, ‘‘Hatuwezi kuruhusu vifaa vya jeshi la Nigeria kuletwa kutoka nje.’’

Zaidi ya Wafugaji miatatu wa CCM warudisha fomu na kuhamia Chadema Monduli.

Zaidi ya wanachama mia tatu wa CCM kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya Engaruka wilaya ya Monduli wamerudisha kadi za CCM na  kujiunga na chadema huku wakidai maamuzi yao yametokana na  utashi wao binafsi kwa kuzingatia hali halisi ya kisiasa ilivyo hivi sasa.
ITV ilifika katika kijiji cha Engaruka na kushuhudia mamia ya wanachama waliyo kusanyika katika mkutano wa hadhara kukusanya kadi za CCM kuzichoma moto  na kuchukua kadi za CHADEMA huku wakiainisha sababu zilizo fanya kufikia maamuzi hayo.

Thursday, 6 August 2015

Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Haruna Lipumba amejiuzulu.

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahimu Haruna Lipumba amejiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho kikongwe hapa nchini.
 
Baada ya minongono ya kutaka kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa kile kilichodaiwa ni maelewano hasi na baadhi ya wakurugenzi wa chama hicho sasa ni rasmi.
 
Prof Lipumba aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo mwaka 1999 kuhusu mchakato wa katiba amesema kwa sasa haoni kama UKAWA utafanikisha upatikanaji wa katiba bora itakayoweza kukidhi  tunu za taifa, utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji, msomi huyo wa mashuhuri wa masuala ya uchumi nchini amesema katika kipindi hiki kabla ya uchaguzi atajikita zaidi katika kuandaa ushauri wa mambo mbalimbali yanayopaswa kutekelezwa na serikali ijayo ambapo baada ya uchaguzi atajikita katika masuala ya kitafiti pekee.

Hatimaye Ndesamburo amfuata Dk. Silaa kwake

Mbunge mstaafu wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo, maarufu kama "Ndesa Pesa", amekutana jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ilielezwa hapo awali na chama chake kuwa kwa sasa yuko mapumzikoni, Dkt. Wilbrod Slaa, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Japan yakumbuka shambulio la Heroshima

Raia wa Japan wamefanya maombi leo
Raia wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Heroshima.
Takriban watu laki moja na arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani kudondosha bomu ambalo liliuharibu mji huo tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 1945.
Watu elfu sabini walipoteza maisha papo hapo, huku wengine wa idadi kama hiyo walipoteza maisha kutokana na athari za mionzi ya sumu.

Chelsea yaichapa Chelsea stamford Bridge

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
Klabu ya soka ya Fiorentiana ya Italia imewachapa mabingwa wa ligi ya England Chelsea kwa bao 1-0.
Bao pekee la ushindi la Fiorentina ama maarufu kama Viola liliwekwa kimiani na beki Gonzalo Rodríguez raia wa Argentina katika Dakika ya 34 baada ya Kipa wa Chelsea Begovic kutema Shuti la Alonso Mendoza.

Bayern Munich mabingwa wa Audi

Kikosi cha Bayern munich
Miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich wametwaa ubingwa wa michuano ya Audi mwaka 2015.
Bayern wakicheza katika uwanja wao Allianz Arena Jijini Munich, wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Real Madrid ya Hispania.

Wednesday, 5 August 2015

Mayweather kupanda ulingoni septemba

Floyd Mayweather
Bondia Floyd Maywether atapanda tena ulingoni mwezi Septemba 12 mwaka huu kuzipiga na Andre Berto.
Floyd atajaribu kuifikia rekodi ya bondia Rocky Marciano, ya kupigana mapambano 49 pasipo kupoteza.Berto ameshinda mapambano 30 huku akipoteza mapambano matatu.

Mawaziri wengine waangushwa kura za maoni

SIKU mbili baada ya mawaziri watano kushindwa katika kura za maoni ya ubunge ndani ya CCM, waziri mwingine, Gaudentia Kabaka anayeshughulikia Kazi na Ajira, naye amedondoshwa katika jimbo la Tarime Mjini.
Kabaka, kabla ya kujitosa katika siasa za majimbo, alikuwa mbunge wa muda mrefu wa viti maalumu. Aidha, katika kura hizo zilizofanyika kote nchini, zimewaacha katika hali mbaya wabunge wanne, baada ya kushindwa katika kura za maoni majimboni mwao.

Tuesday, 4 August 2015

Tetesi za usajili Leo

meneja wa Manchester United Louis van Gaal alitoa dau mara mbili la pauni milioni 100 kutaka kumsajili Gareth Bale, 26, lakini lilikataliwa (Sun), Chelsea wamewaambia Tottenham kutaja bei ya beki wa kushoto Danny Rose, 25- Chelsea wakiwa tayari kutoa pauni milioni 15 (Daily Mirror), Lazio wamemwambia wakala wa Mario Balotelli kuwa wako tayari kumchukua kwa mkopo msimu huu, lakini ikiwa tu watafuzu kucheza Champions League (Daily Mirror), Liverpool huenda wakasubiri hadi siku ya mwisho kabla ya kupata dau kwa wachezaji wake isiyowataka kama Balotelli, Fabio Borini na Jose Enrique (Daily Telegraph), beki wa PSG Thiago Silva anaamini kuwa Angel Di Maria kuhamia Ufaransa ni kupiga hatua kwenda mbele

Kiwanda cha mbu chaanzishwa China

Kiwanda cha mbu chaanzishwa ChinaMbu wa kiume kukuzwa kiwandani kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa kidindapopo

Wanasayansi wa China wameanza kukuza mbu wa kiume kiwandani wanaobeba bakteria kwa ajili ya kuangamiza mbu wengine wanaosababisha ugonjwa wa kidingapopo (dengue).

Mh.Lowasa ameridhiwa kuwa mgombea rasmi wa Ukawa.

Hatimaye mkutano mkuu wa chama cha Democrasia na maendeleo Chadema umeridhia jina la Edward Lowasa kuwa mgombea wa nafasi ya urais huku Bw Juma Duni Haji akipitishwa kuwa mgombea wa nafasi ya makamo wa rais huku Maalim Seif Mahadi akipitishwa kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar.
Ni tambo za ushindi za Edward Lowasa alizozitoa dakika chache baada ya kupitishwa na mkutano mkuu wa Chadema kuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Ukawa na kuvunja minongon iliyokuwa imetanda kuwa Ukawa isingefikia hatua hiyo.
 

Monday, 3 August 2015

Watu milioni 1.6 wamdhamini Lowassa

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akipungia
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akipungia wananchi wakati akiondoka kutoka makao makuu ya Chadema Kinondoni, Dar es Salaam jana, baada ya kurudisha fomu ya kugombea urais kupitia chama hicho

 Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema idadi hiyo ya wadhamini inaashiria ushindi wa kishindo, kwa maelezo kuwa inakaribia idadi ya kura alizopigiwa katibu mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alipogombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


Kada mpya wa Chadema, Edward Lowassa jana amerejesha fomu ya kuwania urais, huku akifanikiwa kupata wadhamini milioni 1.6, zaidi ya nusu ya kura za urais ambazo chama hicho kilipata kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema idadi hiyo ya wadhamini inaashiria ushindi wa kishindo, kwa maelezo kuwa inakaribia idadi ya kura alizopigiwa katibu mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alipogombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Katika Uchaguzi huo, Dk Slaa alishika nafasi ya pili baada ya kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34, huku Rais Jakaya Kikwete akipata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17.
Lowassa alipochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, kabla ya kuhamia Chadema, alidhaminiwa na wanachama 870,000 nchi nzima.
Dk Slaa, ambaye hajaonekana hadharani tangu Lowassa ajiunge Chadema, jana hakuwapo kwenye ofisi za chama hicho wakati mbunge huyo wa Monduli alipokuwa akirejesha fomu.

Hatimaye Dr. Silaa kuanza kuhudhuria vikao vya chadema na Ukawa

Hatimaye katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa kesho ataanza rasmi kuhudhuria vikao vya chama ambapo atahudhuria kikao cha kamati kuu ya Chadema.
Kuonekana kwa Dr. Slaa kesho kutamaliza rasmi mjadala wa muda mrefu na propaganda zilizotawala eti Dr. Slaa kajitoa Chadema.

Azam bingwa mpya wa Cecafa

Azam ilicheza mchezo wa Fainali kombe la CEcafa
Timu ya soka ya Azam Fc ya Tanzania imeutwaa ubingwa kwa kombe la Cecafa kagame Cup kwa mwaka 2015.
baada ya kuichapa timu ya Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainalia uliofanyika katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam Tanzania.
Mabao ya Azam maarufu kama wanalambalamba yalifugwa na washambuliaji wake John Bocco na Kipre Tchetche aliyepiga mpira wa adhabu nakuzama moja kwa moja nyavuni.

Mh.Makongoro Mahanga ametanga kukihama chama cha CCM na kuhamia Chadema.

Siku moja baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura za maoni ndani ya CCM na kushindwa, mbunge wa jimbo la Segerea Mh Makongoro Mahanga ametanagza kukihama chama cha CCM na kujiunga na chama cha Chadema baada ya kutokutendewa haki katika mchakato huo.
Ukandamizaji wa democrasia ndani ya CCM, ni moja ya sababu zilizomfanya naibu huyo wazir wa kazi na ajira kuamua kukikacha chama chake cha CCM, lakini wadadisi wa siasa za Tanzania wanabashiri huenda hii ikawa miongoni mwa sababu kuu.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Dkt Militon Makongoro Mahanga amesema kushindwa kwake kwenye kura za maoni kunatokana na hujuma na upendeleo uliofanywa na uongozi wa CCM wilaya ya Ilala kwa moja ya mgombea wa nafasi hiyo.
Anasema baada ya kujiridhisha nambinu zote chafu zilizotumiwa na baadhi ya wagombea dhidi yake, na pia kujiridhisha bila shaka na namna viongozi wa CCM wanavyompiga vita tangu mwaka 2000 sasa anasema inatosha.
Katika mkutano huo pia amekiri kuwa na mahusiano ya akribu na waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowasa nakwamba kama viongozi wa Chadema watamkubali anaamini atakuwa sehemu salama zaidi katika harakati zake za kisiasa hapa nchini.

Basata yamfungia Shilole kwa utovu wa nidhamu

Shilole amekumbwa na dhahama hiyo baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha akicheza jukwaani akiwa katika mavazi yanayokinzana na maadili ya Kitanzania akiwa nchini Ubelgiji.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole kujihusisha na shughuli za sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Mwanamuziki huyo anayejulikana pia kama Shishi Baby amekumbwa na dhahama hiyo baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha akicheza jukwaani akiwa katika mavazi yanayokinzana na maadili ya Kitanzania akiwa nchini Ubelgiji.