Watu 13 akiwamo mke wa Jaji, Profesa John Luhangisa, Retisia
Luhangisa ambaye ni Ofisa Elimu wa Taaluma wa Halmashauri ya Meru mkoani
hapa, wamefariki duniani baada ya gari la abiria aina ya Hiace
walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.
Katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru maelfu
walifurika kwa ajili ya kutambua jamaa zao ambapo mke na mume ambao ni
Elly Kaaya, Ofisa Elimu na Kumbukumbu wa Halmashauri ya Meru na mumewe
Kundaeli Kaaya ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Ndoombo wilayani
Arumeru walikuwa ni miongoni mwa maiti zilizotambulika katika ajali
hiyo.
Tukio hiilo limetokea jana eneo la Madila kwenye
Kijiji cha Sing’isi saa 10 jioni baada ya gari hilo la abiria lililokuwa
linatokea Usa River kwenda Arusha kugongana na lori hilo lililokuwa
linatoka Arusha kwenda Kilimanjaro.
Wengine waliotambuliwa katika ajali hiyo ni pamoja
na Ofisa Elimu wa Taaluma Halmashauri ya Meru, Zakia Katunga na
kondakta wa gari hilo, Simon Wilenya na abiria Kundaeli Kadoya pamoja na mwanafunzi wa chuo kikuu cha maendeleo ya jamii Tengeru (CDTI-TENGERU) aliyefahamika kwa jina la Loretha Baruti wa mwaka wa Kwanza ambae alikuwa na mwanafunzi mwenzake ambaye yuko kwenye vyumba vya wagonjwa mahutihuti katika hospitali ya Mount Meru jina lake halijafahamika kwa haraka lakini ni Mwanafunzi wa CDTI-TENGERU, pi
Hadi jana jioni, miili mingine sita ilikuwa bado
haijatambulika, huku mamia ya watu wakiendelea kufika katika uwanja wa
chumba cha kuhifadhi maiti kutambua miili hiyo.
Hata hivyo, hadi jana dereva wa gari la abiria
alikuwa hajulikana alipo na majeruhi wengine watatu walikuwa wamelazwa
wakiwa mahututi Hospitali ya Wilaya ya Meru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kesho (leo) angetoa
taarifa ya tukio hilo.
Jaji Luhangisa aliteuliwa hivi karibuni, kuwa Jaji na Rais Jakaya Kikwete.
Kabla ya uteuzi huo, alikuwa msajili wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
No comments:
Post a Comment