Baadhi ya wananchi wamelalamikia mabadiliko ya gharama za utoaji
huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa madai kuwa
wanaumia kutokana na kuwa na vipato vidogo.
Mabadiliko hayo yaliyotangazwa hivi karibuni kwa
wagonjwa wa rufaa ni malipo ya kitanda ya Sh5,000 na Sh2,000 ya chakula
kwa siku.
Akizungumza jijini hapa jana, Yasinta Mlole alisema alitozwa gharama hizo alipompeleka mgonjwa wake kutoka Morogoro.
Alisema ilimlazimu kulipia gharama hizo kwa sababu mgonjwa wake alipewa rufaa ya kutibiwa katika hospitali hiyo.
“Mgonjwa wangu ana hali mbaya. Kwa kweli hali inakuwa ngumu na sijui atakaa hapa mpaka lini,” alisema.
Naye James Mbela alisisitiza umuhimu wa kuipa
kipaumbele sekta ya afya ili kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote
na watendaji wake wanatimiza wajibu.
Awali, msemaji wa MNH, Aminiel Algaesh alisema
tangu mwaka 2003 wagonjwa walikuwa wakilipa Sh20,000 kwa muda wote
walipokuwa hospitali.
No comments:
Post a Comment