Sunday, 26 October 2014

Timu ya taifa kwa wanawake Nigeria wanyakua ubingwa wa Afrika kwa mara ya saba

Timu ya taifa ya Nigeria kwa wanawake
Nigeria iliicharaza Cameroon na kushinda kombe taifa bingwa barani Afrika miongoni mwa akina dada mjini Windhoek namibia.
Baada ya kufanya mashambulizi kadhaa mwanzoni mwa mechi hiyo,Desire Oparanozie aliipatia Super Falcon bao lao la kwanza katika dakika ya 12 baada ya kupiga mkwaju wa nidhamu. Asisat Oshoala baadaye aliifungia Nigeria bao lao la Pili dakika mbili kabla ya kukamili kwa kipindi cha pili na kufanya mambo kuwa mbili kwa sufuri.
Nigeria imeshindwa kushinda taji hilo mara mbili Pekee tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1991.
Equitorial Gunea ndio washindi wengine wa Kombe hilo mnamo mwaka 2008 na 2012,lakini walishindwa kufuzu katika michuano ya mwaka huu.
Mkufunzi wa cameroon Enoh Ngatchu amesema kuwa kufuzu kushiriki katika dimbala dunia kwa upande wa akina dada kwa mara ya kwanza huenda ukaimarisha mchezo huo miongoni mwa akina dada nchini mwake.
Nigeria na Cameroon tayari walikuwa wamefuzu kushiriki katika kombe la dunia mwaka ujao nchini canada baada ya kufuzu katika fainaliza kombe hilo la Afrika.

No comments: