Taarifa
kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema zaidi ya watu ishirini
wameuawa katika mapigano kati ya wanajeshi na wanamgambo wa kundi la
Boko Haram, licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufanyika ijumaa
iliyopita.
Vurugu zilifanyika siku ya katika mji wa Damboa.
Makubaliano ya kusitisha vita kati ya wanamgambo wa Boko Haram na
serikali ya Nigeria yanatarajiwa kuwaokoa wasichana zaidi ya mia mbili
waliotekwa na kikundi hicho mwezi Aprili mwaka huu.Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema mapigano hayo yameleta hali ya wasiwasi kuhusiana na uwezekano kusitisha mapigano hayo.
No comments:
Post a Comment