Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ameelezea
mambo matano aliyokutana nayo katika gereza la Segerea Dar es Salaam
alipokaa mahabusu kwa saa 24 kwa tuhuma za kuongoza maandamano
yasiyokuwa na kibali Oktoba 4 mwaka huu jijini humo.
Akizungumza jana jijini hapa alisema,akiwa humo
alikutana na wasichana wadogo ambao walimweleza wamefika hapo kutokana
na kudai haki zao, lakini kwa kuwa wamekosa watetezi wamejikuta wakisota
gerezani
Aliongeza: “Mpango wa kupunguza wafungwa wenye
vifungo vifupi vifupi unaonekana kukwama, gereza haliendani na wingi wa
watu waliomo.
“Kuna wasichana wadogo wengi sana, wanaochukuliwa
mikoani kuja kufanya kazi za ndani, wakifika huku wanafanya kazi hizo
lakini mwajili wake anaposhindwa kuwalipa na binti huyu akianza kudai
haki yake mwajiri anambabikia kesi.
Mdee ambaye pia ni Katibu wa Kanda ya Mashariki wa
Chadema alisema kesi za mauaji na wizi zimekuwa zikichelewa, jambo
linalowakatisha tamaa washitakiwa kutokana na kukaa muda mrefu.
“Unakuta mtu kweli anajulikana kaua au mwingine
kaiba, lakini upelelezi wake utachukua miaka mingi ni rai yangu kwamba
umefika wakati uwepo utaratibu wa kupunguza mrundikano’ alisema .
Mdee alisema licha ya gereza kuwa sehemu ya
kurekebisha tabia za watu, lakini hali kama hiyo imegeuka kuwa eneo la
kufundishia mbinu chafu za kibiashara..
Wasichana wadogo wanafundishwa biashara chafu na
waliowazidi umri,wakitoka wanakuwa wamoja na kuanzisha makundi ya
uchangudoa” alisema.
Mbunge huyo alisema Serikali ina kazi kubwa ya kukomesha vitendo hivyo na kwamba alipokuwa mahabusu alijifunza mambo mengi.
“Nilipofikishwa kule ilikuwa imeshafika saa 11
jioni, nililetewa ugali ambao haukuwa umeiva, mchicha wenyewe umekomaa
na kama ni dagaa basi hawaoshwi wakitolewa katika gunia tu, wanapikwa
hivyo hivyo na michanga. Uji ndiyo usiseme sasa fedha za bajeti huwa
zinakwenda wapi kama hali ndiyo hiyo,” alihoji Mdee
Mdee alisema licha ya gereza kuwa sehemu ya
kurekebisha tabia za watu, lakini kwa hali kama hiyo imegeuka kuwa eneo
la kufundishia mbinu chafu za kibiashara.
“Hawa dada zetu wadogo wanaowekwa huko, wanakutana
na mi dada iliyokubuhu mitaani kwa vitendo vya kuendesha biashara ya
ngono, ikikutana na hao inawafundisha hao wasichana mbinu chafu.”
“Unakuta inawaeleza kwamba unajua kule mtaani kuna biashara
ambayo ina lipa kuliko hiyo ya kazi za ndani, hivyo mkitoka tutakwenda
kuwafundisha ni kweli wakitoka wanakuwa timu moja wanaanzisha makundi ya
machangudoa,” alisema Mdee
Aliongeza: “Serikali ina kazi kubwa ambayo
inatakiwa kuifanya kukomesha vitendo hivi, lakini nimefurahi nimewekwa
ndani kwani nimeweza kujifunza kitu nikiwa humo na ninatamani siku moja
nirudi tena ingawa walinitoa mapema ili nisijue siri za humo zaidi.”
No comments:
Post a Comment