Juma kaseja |
Okwi alirejea Simba akitokea Yanga baada ya timu
hiyo ya Jangwani kushindwa kuheshimu mkataba wake ikiwa ni pamoja na
kutommalizia dau lake la usajili kwa wakati, alipogoma ndipo wakamshtaki
Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF) ambalo liliridhia mkataba wake
uvunjwe ajiunge na timu anayoitaka ambayo ni Simba.
Kaseja ambaye ni kipa halali wa Yanga alisaini
mkataba wa miaka miwili ambapo mpaka sasa ameshatumikia mwaka mmoja
utakaokamilika Desemba huku klabu hiyo ikimlipa nusu ya fedha zake za
dau la usajili.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa kipa huyo,
Abdulfatah Saleh, alisema ameshangazwa na Yanga kushindwa kukamilisha
ahadi ya malipo ya kipa huyo ambayo yalikuwa yalipwe tangu Januari 17.
Abdulfatah alisema, tafsiri iliyopo kisheria ni
kwamba Yanga wamekiuka mkataba na huenda ishu ya Kaseja ikawa kama ya
Emmanuel Okwi ambaye Yanga ilikiuka mkataba wake wa malipo akatua Simba.
“Unajua naweza kufananisha hili na lile la Okwi,
unamuahidi mchezaji wako kumlipa fedha zake baada ya muda fulani lakini
hufanyi hivyo akija kukudai unachukia, hatupendezwi na hili tunaona kama
Yanga wamedhamiria kuvunja mkataba kwa kushindwa kumlipa Kaseja fedha
zake mpaka sasa,”alisema Abdulfatah.
“Wakati wanamsaini tulikubaliana kwamba kiasi cha
fedha kilichosalia wanapaswa kutulipa Januari mwaka huu, sasa
tunazungumza huu ni mwezi Oktoba hakuna malipo yoyote, kwetu tunapata
tafsiri tofauti. Angalia hata wanavyomtumia hawampi mechi za kucheza ni
juzi ndiyo kacheza mechi ya kirafiki dhidi ya CDA ya Dodoma.
“Kaseja ni kipa mwenye uwezo mkubwa na hadhi yake sio kumchezesha mechi kama hizo.”
Aidha Abdulfatah alikiri kipa huyo kuhitajika na
wapinzani wao Simba akisema: “Kweli Simba walionyesha nia ya kutaka
kumsajili lakini hatuwezi kuzungumza nao lolote tumewaambia bado Kaseja
ana mkataba na Yanga labda wazungumze nao.”
No comments:
Post a Comment